Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wa kumuoa Kajala bado hajazaliwa

KAJALA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Kajala alisema mbali na wanaume wengi ambao amekuwa akihusishwa nao na hata kupostiwa nao mtandaoni kupitia picha na video, lakini mumewe mtarajiwa wake bado ni siri nzito na hakuna atakayemjua mapema hadi atakapoamua mwenyewe.

MWIGIZAJI wa Bongo Movie, Kajala Masanja amefichua licha ya watu kumhusisha na wanaume wengi tofauti, lakini mwanamume halisi atakayemuoa bado ni siri na hakuna atakayemjua kirahisi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kajala alisema mbali na wanaume wengi ambao amekuwa akihusishwa nao na hata kupostiwa nao mtandaoni kupitia picha na video, lakini mumewe mtarajiwa wake bado ni siri nzito na hakuna atakayemjua mapema hadi atakapoamua mwenyewe.

“Unajua watu wanaona tu mitandaoni, watashangazwa sana na mimi kwa sababu mengi yanayosemwa si ya kweli, lakini siku watasikia tu nishaingia kwenye ndoa na ni mke wa mtu, mume wangu hawawezi kumjua kirahisi,” alisema Kajala Masanja.

Kajala aliongeza pindi atakapoingia katika ndoa, atakuwa tayari kupata mtoto kwani hahofii kama ana mjukuu kutoka kwa mwanae Paula, aliyezaa na Marioo.

"Siyo ajabu mimi sasa hivi kupata mtoto, kwani mimi ndiyo nitakuwa wa kwanza kupata mtoto huku nikiwa na mjukuu? Hivyo nikiolewa mume akitaka mtoto sitaweza kupinga, kwani umri wangu bado unaruhusu ni suala la kumuomba Mungu tu," alisema Kajala Masanja.