Shilole apindua meza, G Nako agusanisha

Sunday August 29 2021
shilole pic
By Thomas Ng'itu

WASANII wa Bongofleva, Shilole na G Nako ni miongoni mwa wasanii ambao tayari wamepiga shoo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa katika kilele cha Wiki ya Mwananchi huku na kuwafurahisha mashabiki.

Shilole ameingia uwanjani hapo na kuimba nyimbo yake iitwayo ‘Pindua Meza’ aliyoiimba kwa kuzunguka uwanjani hapo akiimba sambamba na mashabiki kisha kuondoka.

Baada ya hapo, aliingia G Nako kwa kuimba Ngoma yake iitwayo Gusanisha na mashabiki kuangusha shangwe huku wengine wakiimba naye.

Baada ya Gusanisha, G Nako aliimba nyimbo ya Gere ambayo ni ya kundi lake Weusi kisha kushuka stejini na kuondoka.

Baada ya G Nako kuondoka aliingia Madee ambaye naye aliliamsha jukwaa kwa nyimbo yake ya Hela kisha kuondoka.

Advertisement