Shamsa Ford ana deni la watoto tisa

Muktasari:
- Mwanadada huyo anayefahamika zaidi kwa jina la Chausiku, alilolitumia ndani ya filamu ya Chausiku akiigiza kama binti mcharuko, aliliambia Mwanaspoti kuwa, mumeme ambaye pia ni mwigizaji kama yeye, mara walipooana alimwambia anataka amzalie watoto kumi na anashukuru hadi sasa ameshazaa naye mtoto mmoja wa kike.
MWIGIZAJI nyota wa filamu nchini, Shamsa Ford amesema ana deni kubwa kwa mumewe, Hussein Lugendo 'Mlilo' la kumzalia watoto tisa.
Mwanadada huyo anayefahamika zaidi kwa jina la Chausiku, alilolitumia ndani ya filamu ya Chausiku akiigiza kama binti mcharuko, aliliambia Mwanaspoti kuwa, mumeme ambaye pia ni mwigizaji kama yeye, mara walipooana alimwambia anataka amzalie watoto kumi na anashukuru hadi sasa ameshazaa naye mtoto mmoja wa kike.
"Mimi sasa hivi nina watoto wawili, niliozaa na wanaume tofauti, kati ya hao mmoja nimezaa na mume wangu, Mlilo aliyeniambia anataka nimzalie watoto 10, hivyo kwa sasa nina deni la watoto tisa kuweza kutimiza idadi hiyo aliyoitaka," alisema Shamsa.
Shamsa aliongeza kuwa, kauli hiyo ya mumewe imemfurahisha kwani hata yeye anapenda sana watoto na kilichobakia ni kumuomba Mungu aweze kutimiza hitaji la Mlilo aliyefunga naye ndoa, Agosti mwaka jana baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.