Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Safari ya Banana Zorro kimuziki ilianza na Westlife

FACT Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa ukizungumzia wanamuziki Bongo wenye uwezo mkubwa wa kufanya aina mbalimbali za muziki kama RnB, Pop na Zouk, basi Banana ambaye ni mtoto wa gwiji wa muziki, Zahir Zorro, atachukua nafasi kubwa. Twende nayo.

JINA la Banana Zorro ni lake kabisa na ndilo alipewa na wazazi wake. Jina hilo (Banana) karithi kutoka kwa mmoja wa babu zake na alipoingia kwenye muziki alikuwa halipendi sana, ila baadaye akaja kulikubali hadi katika sanaa.

Kwa sasa ukizungumzia wanamuziki Bongo wenye uwezo mkubwa wa kufanya aina mbalimbali za muziki kama RnB, Pop na Zouk, basi Banana ambaye ni mtoto wa gwiji wa muziki, Zahir Zorro, atachukua nafasi kubwa. Twende nayo.


1. Miongoni mwa waimbaji wakubwa duniani waliomvutia Banana kimuziki naye kutaka siku moja kufikia hatua hiyo, ni Michael Jackson ambaye hadi sasa ameuza rekodi zaidi ya milioni 400 duniani, huku akishinda tuzo 15 za Grammy kipindi cha uhai wake.


2. Mwaka 2001 ndipo Banana alishiriki mashindano ya Tanzania Pop Idol akaibuka mshindi na kuwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika huko Afrika Kusini. Aliimba nyimbo za wasanii wa nje kama Westlife kwa ustadi mkubwa hadi majaji kumpa ushindi.


3. Baadaye alikuja kusainiwa Smooth Vibes chini ya Prime Time Promotion na kufanya makubwa. Rekodi lebo hii ndio iliwatoa mastaa wengine wa Bongofleva akiwemo Lady Jaydee na Ray C ambao awali walikuwa wakitangaza redioni.


4. Akaja kukutana na Miikka Mwamba, mtayarishaji muziki kutokea nchini Finland ambaye ndiye alitengeneza wimbo wake maarufu, Mama Yangu (2003) akimshirikisha D Knob na ndio uliobeba jina la albamu yake ya kwanza.


5. Miikka Mwamba alibadilisha kila kitu ambacho Banana alitaka kiwepo katika wimbo huo, akamwambia tulia nikupe ngoma kali (hit), akajifungia studio zaidi ya saa mbili akitengeneza mdundo kisha akamuita Banana arekodi na ulipotoka ukawa historia.


6. Ikumbukwe Miikka Mwamba tangu mwaka 1999 aliajiriwa FM Studio kama mtayarishaji muziki hadi 2004 ulipomalizika mkataba wake akiwa ametengeneza nyimbo kibao kali nyingi zenye historia katika Bongofleva.

Kati ya hizo ni Mama Yangu (Banana Zorro), Babygal (Mad Ice), Kamanda (Daz Nundaz), Kwenye Chati (Balozi Dola Soul), Mkiwa (K Sal), Kitu Gani (D Knob), Mpenzi (Dudu Baya), Maria Salome (Saida Karoli), Tamala (Hardmad), Eno Maiki (Ziggy Dee) na kadhalika.


7. Mbali na Miikka Mwamba, watayarishaji wengine Bongo ambao Banana alifurahi kufanya nao kazi ni Bizman, Allan Mapigo na Enrico Figueiro kutoka Sound Crafters. Kwa miaka mingi Banana aliaamini kuwa muziki wake umewafaa zaidi watayarishaji hao, hivyo kila wakifanya kazi lazima iwe nzuri na kweli nyimbo walizotoa pamoja ni bora kwa muda wote.


8. Wimbo wake, Nipo Radhi (2006) Banana aliurekodi kwa free style tu yaani alikuwa studio na Allan Mapigo akapiga mdundo wake alipousikia tu, hapo hapo akaanza kuimba hadi akamaliza kurekodi.


9. Ngoma hiyo kutoka katika albamu yake ya pili, Subra (2006) ilishinda tuzo ya TMA kama Wimbo Bora wa RnB, kiitikio chake kwa asilimia kubwa Banana amesaidiwa na Allan Mapigo, hivyo hata anapokuwa akiutumbuiza sehemu hiyo huwa inampa shida kidogo.


10. Hata hivyo, tuzo ya kwanza Banana kushinda Bongo ilikuwa ya TMA 2003 kama Msanii Bora wa Kiume baada ya kufanya vizuri na albamu yake ya kwanza, huku Stara Thomas akishinda kama Msanii Bora wa Kike. Ikumbukwe Stara Thomas aliyetoka na albamu yake, Nyuma Sitorudi (2000), tuzo yake ya pili ya TMA ilikuwa mwaka 2010 katika kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana (Nipigie) akiwa na AT, mwanachama zamani wa kundi la Offside Trick.