Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzee Yusuf, mkewe wala hakuna cha siri

MZEE Pict

Muktasari:

  • Mzee na Leila ambaye pia ni mwimbaji nyota wa miondoko hiyo ya taarabu, ni moja ya wanandoa waliodumu pamoja huku wakiendeleza sanaa yao ya muziki, tofauti na ilivyo kwa mastaa wenye majina kama wao.

MFALME wa muziki wa taarabu nchini, Mzee Yusuf amefunguka kitu kikubwa kilichomfanya adumu miaka mingi na mkewe, Leila Rashid ni kutofichana mambo.

Mzee na Leila ambaye pia ni mwimbaji nyota wa miondoko hiyo ya taarabu, ni moja ya wanandoa waliodumu pamoja huku wakiendeleza sanaa yao ya muziki, tofauti na ilivyo kwa mastaa wenye majina kama wao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mzee alisema licha ya kupitia ‘mishale’ mingi katika uhusiano huo na mkewe, kilichowabeba ni kukwepa kuficha mambo yao, yaani kwao hakuna cha siri baina yao.

“Unajua mke wangu amekuwa akisikia mengi sana, lakini kwa kuwa nikirudi nyumbani simfichifichi wala sina makandokando, ananiamini sina mchepuko,” alisema Mzee.

Mzee Yusuf alioana na Leila mwaka 2004 hadi kwa mwaka huu wanandoa hao wamefikisha miaka 21 katika ndoa hiyo, huku kila mmoja akiendelea na shughuli ya muziki.