Rick Ross kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro

Rick Ross kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro

Rapa wa Marekani, Rick Ross amefika juu ya kilele cha mlima wa Kilimanjaro baada ya watu wawili kwenda na picha yake kwenye kilele cha mlima huo.

Watu hao wameonekana kushika picha ya staa huyo ambapo chini imeandikwa ‘Welcome to Tanzania'.

Picha hiyo imewekwa pia katika ukurasa wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kueleza kuwa wapo tayari kwa ajili yake.

Rick Ross hivi karibuni amekuwa gumzo nchini Tanzania baada ya kuonekana nchini Dubai wakiwa wanakula bata na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Hata aliporejea nchini, Hamisa aliwaeleza waandishi namna gani msanii huyo anavyoipenda Tanzania na kueleza nia yake ya kuja kuwekeza nchini.

Kwa ukaribish0 huo wa Tanapa na Rick kuonyesha kuukubali kwa kuweka picha hiyo kwenye ukurasa wake na emoj ya asante ni wazi kwamba Tanzania itarajie ugeni wake siku yoyote.

Msanii huyo ni moja ya marapa matajiri duniani ambapo kwa mujibu wa jarida la biashara la kimarekani la Forbes ana utajiri wa dola milioni 42 hadi kufika mwaka 2021 na kushika namba 35 kati ya marapa 99  wenye utajiri mkubwa wa kifedha, huku Jay Z akishika nafasi ya kwanza kwa utajiri wa dola bilioni moja.