Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rich Richie kumbe naye amejipanga

SIKU chache baada ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), mwigizaji Single Mtambalike ‘Rich Richie’ amesema katika utekelezaji wa majukumu yake hataleta ushabiki badala yake ni kuchapa kazi tu.

Richie aliyepokea kwa furaha uteuzi hio na kumshukuru Waziri mwenye dhamana ya sanaa, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema kazi aliyopewa ataifanya kwa weledi na si kishabiki kwa vile kuna mambo mengi ya kutekelezwa kwa afya ya sanaa ya Tanzania.

“Nitafanya kazi kulingana na muongozo wa Bodi sawa na wengine, kazi hii inahitaji weledi hivyo sintofanya kishabiki kwa maana ya kutafuta kiki na vitu vingine, naaomba Mungu aniongoze,” alisema Richie.

Moja ya jambo alilopanga kuliangazia kama ni sehemu ya wajumbe wa Bodi ni kuhakikisha anapigania na kutoa elimu ili vijana na jamii nzima ikaacha kulemaa na utandawazi na kurejea katika kuimarisha mila, desturi na tamaduni za Kitanzania kwani ni biashara kubwa ambayo haijatangazwa vya kutosha.