Rayvanny aiteka Chamazi Complex

Rayvanny aiteka Chamazi Complex

Msanii wa kizazi kipya aliyeaga kwenye lebo ya WCB, Rayvanny amefanya shoo amewateka mashabiki katika Uwanja wa Azam Complex kwa burudani kali aliyotoa.

Rayvanny aliingia katika Uwanja wa Azam Chamazi saa 11:43 jioni akiwa na staili ya aina yake ambayo haikutegemewa na wengi waliokuwa hapa uwanjani.

Msanii huyo aliingia na gari 15 aina ya V8 zilizokuwa zimefuatana na Brabus Mercedes-Benz pamoja na Benz Local alilokuwa amepanda Rayvanny.

Baada ya kufika uwanjani eneo la kuchezea Rayvanny alikiwa na walinzi wake kumi nyuma aliibua shangwe la mashabiki na kuanza kumshangilia.

Baada ya kushuka mbali ya walinzi wake alikuwa na madansa si chini ya 60, aliokuwa nao akiimba na kucheza kwa pamoja.

Rayvanny alifanikiwa kusherehesha kwa kiasi kikubwa kwa kuamsha shangwe na mashabiki aliokuwa akiimba nao pamoja katika nyimbo zake.

Baada ya kufanya shoo hiyo ya dakika 30, Rayvanny alirudi kwenye gari alilokuja nalo kisha kuondoka uwanjani.