Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rambo athibitisha ujio wa Creed 2

Muktasari:

  • Ijumaa ya wiki iliyopita katika akaunti yake ya Instagram, Rambo aliweka picha yake pamoja na Michael wakitokea katika moja ya kipande katika filamu hiyo na kuweka maneno haya ““Getting stronger !!! 2018″ akiambatanisha na hashtags za #Creed 2 #mgm #fitness #Rocky na hiyo kutoa picha ya wazi juu ujio wa sehemu ya pili ya filamu hiyo.

Dar es Salaam. Mcheza filamu Sylvester Stallone “Rambo” amethibisha ujio wa filamu ya Creed sehemu ya pili katika msimu wa kwanza alishiriki yeye pamoja na Michael B Jordan.

Ijumaa ya wiki iliyopita katika akaunti yake ya Instagram, Rambo aliweka picha yake pamoja na Michael wakitokea katika moja ya kipande katika filamu hiyo na kuweka maneno haya ““Getting stronger !!! 2018″ akiambatanisha na hashtags za #Creed 2 #mgm #fitness #Rocky na hiyo kutoa picha ya wazi juu ujio wa sehemu ya pili ya filamu hiyo.

Kampuni iliyoandaa filamu hiyo MGM ilithibitisha suala hilo ambapo moja ya waandaaji alisema kuwa sehemu ya pili ipo katika maandalizi bado ya awali na inategemewa kukamilika mwakani.

Filamu ya Creed iliyoachiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 ilifanya vizuri sokoni kwa kuingiza dola za kimarekani milioni $173 huku Rambo akishinda Best Supporting Actor katika tuzo za Golden Globe Awards.

Filamu ya Creed ni muendelezo mpya wa filamu ya zamani ya Rambo inayojulikana kwa jina la Rocky iliyotolewa kwa kwanza mwaka 1976 na kushinda katika tuzo za Oscar katika vipengele vya Best Acting na Best Original Screenplay.

Julai mwaka huu Rambo aliweka picha huku akisema ashamaliza kurasa 120 kuandika huku akithibitisha katika msimu huo mpya, uhusika wa Dolph Lundgreen utarudi tena na ikumbukwe katika filamu ya Rocky 4, Dolph ndiye alimuua Baba yake na Addonis “Appollo Creed” mwenyewe na hivyo kuzidi kuibua hisia zaidi kwa wapenzi wa filamu duniani jinsi itavyokua katika sehemu ya pili.

Mpaka sasa ushiriki rasmi wa wahusika wengine haujafahamika, lakini kuna matumaini makubwa ya kuonekana tena kwa Rambo na Michael B Jordan kusimamia shoo.