Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni bifu tena! Kauli ya Diamond kwa Alikiba ina maana gani?

WASANII wa Bongofleva kutokea Kings Music na WCB Wasafi, Alikiba na Diamond Platnumz wameendelea na mvutano wao na sasa hawachaguliani maneno ya kutupiana mtandaoni, kila mmoja anajiona bora na kumshusha mwenzake kimuziki. 

Bifu lao limeibuka tena hivi karibuni baada ya Diamond kutangaza ujio wake mpya ulioambatana na ngoma tano, Shu!, My Baby na Enyoy akishirikiana na Jux; Yaya akishirikiana na Rayvanny na Jux; na Tuna Kikao ft Lavalava, huku akisema ujio wake huo utatawala chati za muziki hadi Januari 2024.

Ni kauli ambayo Alikiba aliipinga vikali na kuamua kuachia wimbo wa Amapiano kwa mara ya kwanza, Sumu akimshirikisha Marioo, kisha ikafuata ngoma ngingine, Love Song akishirikiana na Marioo tena.

Hata hivyo, nyimbo hizi hazijafanikiwa kukamata nafasi ya kwanza YouTube na kumuondoa hapo Diamond hadi pale Zuchu alipofanya hivyo kupitia wimbo wake mpya, Honey kitu ambacho Diamond amemzodoa nacho sana Alikiba.

Alikiba anamkejeli Diamond kwa kumuita “Kwevo” akiwa na maana ya “Quavo”, Rapa wa kundi la Migos kutokana na kuiga mtindo wake wa nywele na mavazi, kubwa zaidi anadai kuwa Diamond hapendi maendeleo ya wenzake!

“Roho inakufukuta kutwa Insta story, halafu inabidi uzoee kuhusu ngoma mfululizo (kali), vinginevyo roho yako chafu itakutia msongo wa mawazo...” amesema Alikiba na kuongeza.

“Fedha unazowekeza kuletea figisu mitikasi ya wenzio ungeenda kujifunza kuimba ili uache wivu na kugandamizia (kukopi), sema najua unaikubali sana ‘Sumu’, kuna hii ‘Love Song’ isikilize kali sana.” ameeleza Alikiba.

Basi Diamond akaona Alikiba ameinua mapanga tayari kwa vita, akageuka nyuma na kuchukua mabomu na vifaru kabisa, kauli zake kwa Alikiba akijibu hilo zinaachana maswali kibao ila tutazichakata hapa. 

“Wewe umewekeza kwenye production gani? wakati video yangu moja ni sawa na video zako 20, audio yangu moja ni sawa na audio zako 20, tatizo unaokaa nao hawakwambii ukweli, wanakudanganya.” amejibu Diamond.

Je, ni kweli video moja ya Diamond ni sawa na video 20 za Alikiba? Tunaweza kupata picha ya hili kuangalia gharama za baadhi ya video zao ambazo wao wenyewe waliziweka wazi kwa mashabiki wao.

Kwa mujibu wa Babu Tale, video ya wimbo wa Diamond, Nana akimshirikisha Mr. Flavour wa Nigeria, iligharimu Dola40,000, wastani wa Sh98.1 milioni kwa sasa, video hiyo iliyotoka Mei 29, 2015 ilifanyika Cape Town, Afrika Kusini na Director Godfather.

Naye Alikiba alieleza video yake iliyowekeza fedha nyingi ni ya wimbo, Aje ambayo iligharimu Dola32,000, wastani wa Sh78.5 milioni, video hii ilitoka Mei 19, 2016 ikiongozwa na Director Meji na ilifanyika Cape Town, Afrika Kusini pia.

Haya tuchakate mambo, kama video moja ya Alikiba ni sawa na video 20 za Diamond, na huyu Alikiba anafanya video kwa Dola32,000, inamaana tuchukue Dola32,000 tuzidishe mara 20 ndio tupate thamani ya video moja ya Diamond kama alivyodai!.

Ukizidisha hapo unapata Dola640,000, wastani wa Sh1.5 bilioni, kusema Diamond anaweza kufanya video kwa gharama hiyo utakuwa ni uongo, hata akiwa na fedha hizo hawezi kuwa na uthubutu huo kutokana soko lake haliruhusu.

Hata hivyo, Alikiba kwa upande wa video kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa hafanyi zile video za kushtua kama hapo awali, na hii ni baada ya kuachana na RockStar Africa na Sony Music ambapo alitoa video kali kama Mwana, Aje, Seduce Me n.k

Akiongea na Podcast ya Swahili Radio by Audomack, Alikiba alisema gharama za kutayarisha video ni kubwa hadi kufikia Dola35,000, wastani wa Sh85.8 milioni ila uwekezaji huo haurudi na hata ukirudi inakuwa kwa kuchelewa sana.

“Ndio maana nilikuwa nasema watu wasishangae baadaye kuona tumebadilika, tunauza tu muziki (audio) maana ndipo tunaingiza fedha, bajeti ya video tunawekeza kiasi kikubwa lakini kinachelewa kurudi.” alisema Alikiba.

Kauli hiyo aliyoitoa Alikiba miaka miwili iliyopita, inasadifu kile ambacho kinaendelea katika muziki wake kwa sasa, tangu mwaka huu umeanza ameachia nyimbo nne, Mahaba, La La La, On Fire na Sumu ila ni wimbo mmoja tu (Sumu) ndio ametoa video yake rasmi!.

Wakati Diamond ameachia nyimbo nne, Yatapita, Zuwena, Shu! na My Baby na zote ametoa video zake rasmi na zimefanya vizuri, mfano Yatapita na Zuwena zilizotoka mwanzoni mwa mwaka, zimefikisha ‘views’ zaidi milioni 20 YouTube.

“Nimekukuta kwenye muziki na nimekupita kila kitu, kimauzo, tuzo, followers, subscribers, viewers, listerners, bei za show, kimaendeleo, kifupi kila kitu.” kauli ya Diamond kwenda kwa Alikiba. 

Kauli hii ya Diamond ina ukweli kwa asilimia kubwa lakini hakuna ubaya kwa mtoto kumzidi mafanikio mzazi wake, Diamond ni mtoto kimuziki kwa Alikiba kwa sababu ana mchango katika kutoka kwake kimuziki.

Ikumbukwe Alikiba ndiye aliyetoa ruhusa ili Diamond arekodiwe wimbo na Prodyuza Bob Junior kwa kuwa alikuwa katika uongozi wa Sharobaro Records iliyomtoa Diamond kimuziki baada ya kuachia nyimbo kama Mbagala na Kamwambie iliyobeba jina la albamu yake ya kwanza.