Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Naye Marioo kamtosa Anjella kama Christian Bella

KAMA ni sauti tu ya uimbaji, basi Anjella amebarikiwa hadi kuivutia Konde Music Worldwide yake Harmonize kumsaini akiwa ni msanii wa kwanza wa kike kusainiwa na lebo hiyo aliyofanya nayo kazi kwa takribani miaka mitatu.

Licha ya kutoachia albamu wala EP na kutoshinda tuzo yoyote hadi sasa, bado Anjella yupo kundi la wasanii waliofanya vizuri kipindi cha miaka mitano iliyopita, namba zake kwenye mitandao zinathibitisha hilo. Fahamu zaidi.


1. Awali Anjella alishiriki mashindano ya uimbaji na kukamata nafasi ya tatu, utakumbuka kuna waimbaji wakubwa wa kike Bongo nao waliwahi kushiriki mashindano mbalimbali ila hawakuibuka washindi, miongoni mwao ni Nandy na Zuchu.


2. Harmonize aliomba mashabiki kumpendekeza msanii wa kike ambaye atamshirikisha katika wimbo wake, ndipo mashabiki wengi wakampendekeza Anjella, Harmonize alikuwa hamjui ila akaanza kumfuatilia kupitia YouTube na kuridhika na uwezo wake.

Na muda mfupi baadaye, Anjella akasikika katika Wimbo wa Harmonize, All Night ambao ulitoka Februari 16, 2021, wakati huu bado alikuwa hajasainiwa Konde Music.


3. Muu Kinanda ndiye alianza kurekodi nyimbo za wasanii wengine walizokuwa wanarudia (cover) Anjella na baadaye kuja na wazo la yeye kuimba katika masoko mbalimbali Dar es Salaam kama Tandika baada ya kufanya hivyo Kiwalani kwa muda.


4. Kwa mara ya kwanza Anjella anaonana na Harmonize alikuwa amefuatana na baba yake mzazi George, hiyo ni baada ya kupigiwa simu na kuitwa katika ofisi za Konde Music na mengine baada ya hapo ni historia.


5. Mshindi wa Tuzo za muziki Tanzania (TMA) 2022 kama Msanii Bora Chipukizi wa Kiume, Kontawa ndiye aliyeandika Wimbo wa Anjella, Respect (2023) ambao ndio wa mwisho kuachiwa kutoka kwake.


6. Baada ya kusainiwa Konde Music ilimchukua Anjella miezi mitatu tu kufikisha wafuasi (subscribers) 100,000 katika chaneli yake ya YouTube na kupatiwa tuzo ((Silver Button) na mtandao huo kama ilivyo kwa wazalisha maudhui wengine. 

Ikumbukwe Zuchu ndiye anashikilia rekodi Afrika kama msanii aliyepata ‘subscribers’ 100,000 ndani ya muda mfupi, huyu baada ya kusainiwa WCB Wasafi ilimchukua wiki moja tu kufikia namba hizo.


7. Anjella ndiye msanii pekee wa kike aliyeshirikishwa katika albamu ya pili ya Harmonize, High School (2021), hii ni tofauti na albamu ya kwanza ya Harmonize, Afro East (2020) ambayo ilishirikisha wasanii wawili tu wa kike, Lady Jaydee na Yemila Alade.


8. Tangu ametoka kimuziki, Anjella ameshirikisha wasanii wawili tu katika nyimbo zake, nao ni Harmonize na AT, mkali wa mduara aliyevuma na Kundi la Offside Trick kutokea Zanzibar, huyu amesikika katika wimbo, Saizi Yako (2021).


9. Hadi sasa Anjella ndiye msanii pekee wa kike Bongo aliyeshirikiana zaidi na Harmonize kwa muda wote, wawili hao wameshirikiana kwenye nyimbo tano ambazo ni; All Night, Kama, What Do You Miss, Kioo na Toroka.


10. Sauti ya kike inayosikika katika Wimbo wa Marioo, Naogopa (2022) akimshirikisha Harmonize ni ya Anjella ingawa hajatajwa kushiriki katika ngoma hiyo wala kwenye video hajaonekana.

Hiyo ni sawa na wimbo wa Christian Bella, Ollah (2017) akiwa na Khalighraph Jones kutokea Kenya, kuna sauti za Ruby na Nandy ambao nao hawajatajwa kama wameshiriki katika wimbo huo uliotengenezwa na Kadric, huku video ikisimamiwa na Hanscana.