Mzee Matata wa Mizengwe afariki dunia

Muktasari:

  • Muigizaji wa vichekesho wa kundi la Mizengwe, Jumanne Alela maarufu kwa jina la Mzee Matata amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa anapatiwa matibabu.

Muigizaji wa vichekesho wa kundi la Mizengwe, Jumanne Alela maarufu kwa jina la Mzee Matata amefariki dunia.

Taarifa ya kifo chake zimethibitishwa leo Jumatano Juni 15, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha.

Aligaesha amesema msanii huyo amefariki dunia jana saa tano na nusu usiku wa kuamkia leo.

“Msanii Bw. Jumanne Alela amefariki dunia jana saa tano na nusu usiku wa kuamkia leo. Alilazwa tarehe 13.6. 2021” amesema Aligaesha

Enzi za uhai wake Mzee Matata alitamba na maigizo katika kikundi cha Mizengwe kilichokuwa na wasanii, Mkwere Original, Safina, Sumaku na Maringo Saba.