Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvungi: Mapenzi na H.Baba tupo mubashara

Muktasari:

  • Muigizaji huyo ambaye mama wa watoto wawili amedai bado yupo kwenye ndoa na mumewe H.Baba lakini kwa sasa hawaishi pamoja kutokana na H.Baba kubadirisha bihashara na anaifanyia jijini Mwanza huku yeye akiishi na watoto jijini Dar.

Msanii wa filamu Flora Mvungi amewajibu wale watu waliokuwa wakidai kuwa ameachana na mumewe ambaye ni mwanamuziki H.Baba, kwamba hawajaachana na hakuna mategemeo ya aina hiyo.

 

Muigizaji huyo ambaye mama wa watoto wawili amedai bado yupo kwenye ndoa na mumewe H.Baba lakini kwa sasa hawaishi pamoja kutokana na H.Baba kubadirisha bihashara na anaifanyia jijini Mwanza huku yeye akiishi na watoto jijini Dar.

 

Flora amesema,hiyo ndio inayowapata maneno maneno watu na kuzua kuwa wameachana,lakini wameshajipangia kila baada ya mwisho wa wiki au mwisho wa mwezi huwa wanatembeleana.

 

"Hili swali naulizwa sana jamani,mimi sijaachana na H.Baba,na najua hizi habari zinatokana na sisi kuishi tofauti tofauti,maana sasa hivi H.Baba anaishi Mwanza kuna bihashara tumefungu kule,na mimi naishi Dar es Salaam na watoto na kazi zangu nyingi nazifanyia hapa Dar,hivyo ndio maana watu hawatuoni pamoja na kuanza kuzua zua,ila wenyewe tushajipangia huwa tunatembeleana kila baada ya mwishoni mwa wiki au mwisho wa mwezi"Alisema Frola