Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MUSIC FACTS: Mandojo na Domokaya wamnunulia Madee kiwanja Sh500,000

Muktasari:

  • Walianza kupambania ndoto zao tangu wapo sekondari, muziki ndilo lilikuwa chaguo lao la kwanza katika haya maisha, kwa yale waliyofanya katika tasnia hiyo ni wazi hawakukosea kuchagua upande huo. Fahamu zaidi.

Ni moja ya makundi yaliyodumu kwa muda mrefu katika Bongo Fleva, Mandojo na Domokaya kwa miaka yote muziki wao umebeba ujumbe wenye hisia kali zinazochagizwa na mpangilio mzuri wa sauti zao.

Walianza kupambania ndoto zao tangu wapo sekondari, muziki ndilo lilikuwa chaguo lao la kwanza katika haya maisha, kwa yale waliyofanya katika tasnia hiyo ni wazi hawakukosea kuchagua upande huo. Fahamu zaidi.


1. P-Funk Majani alikutana na Mandojo na Domokaya akiwa kwenye ziara (tour) ya albamu ya pili ya Juma Nature, Ugali (2003) Arusha na alivutiwa na uwezo wao na kuwakaribisha Bongo Records kwa ajili ya kufanya kazi.


2. Walipofika Dar es Salaam kutokea Arusha walifikia Vingunguti na waliibiwa baadhi ya vitu vyao kama viatu kabla ya kufika Bongo Records, ndipo walikotoka kimuziki.


3. Wimbo wa kwanza kurekodi kwa Majani ni ‘Nikupe Nini’ ambao ndio uliwatoa kimuziki na ulijumuishwa katika albamu yao ya kwanza, Taswira (2005) iliyokuwa na nyimbo nyingine kali kama ‘Digi’, ‘Wanok Nok’, ‘Niaje’ n.k.


4. Kwa mara ya kwanza walitumbuiza wimbo wao ‘Nikupe Nini’ katika show ya Professor Jay ‘Mapinduzi Halisi’ iliyofanyika Arusha, na ndio ilikuwa siku ya kwanza kuusikia wimbo huo baada ya Majani kumaliza kazi yake.


5. Wimbo wa Mwana FA, Kama Zamani (2013) akiwashirikisha Mandojo na Domokaya na Kilimanjaro Band (Njenje) ulirekodiwa kwa watayarishaji muziki watatu, kwa Marco Chali, Bob Manecky na P-Funk Majani ambaye toleo lake ndilo liliachiwa.

Na ‘Kama Zamani’ ndio wimbo uliomfanya Hamisa Mobetto, Miss XXL After School Bash (2010) kuanza kuwa shabiki wa Mwana FA ‘Hamis Mwinjuma’ ambaye sasa ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.


6. Mandojo na Domokaya walirekodi wimbo wa Professor Jay ‘Wapi Nimekosea’ kutoka katika albamu ya J.O.S.E.P.H (2006), siku chache kabla ya wao kusafiri kwenda Uingereza kwa mara ya kwanza.


7. Walitaka kuacha kurekodi hadi warudi ila marehemu Gardner G. Habash akasisitiza warekodi kabla ya kwenda huko Uingereza na walitumbuiza katika hafla ya Miss Tanzania Uingereza.

Ikumbukwe Mh. Temba na Chege kutoka TMK Wanaume safari yao kwanza Uingereza na Dubai ilikuja baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Dar Mpaka Moro’ ambao Chege ndio aliuandika.


8. Wimbo wa Madee, ‘Kazi Yake Mola’ akiwashirikisha Mandojo na Domokaya ndio uliobeba jina la albamu yake ya kwanza ambayo ndio iliyompatia fedha za kununua kiwanja chacke cha kwanza kwa Sh500,000.


9. Video ya wimbo wa Mandojo na Domokaya ‘Nikupe Nini’ imetoka baada ya miaka 17 ya kuachiwa wimbo huo, video ilitoka rasmi Oktoba 7, 2020 ikiongozwa na Director Ez Brown.


10. John Dilinga maarufu kama DJ JD ndiye aliwapigia simu Mandojo na Domokaya na kuwaomba washiriki katika wimbo wa K Sal ‘Starehe na Fedha’ ambao ulitengenezwa na Miikka ‘Mwamba’ Kari kutoka nchini Finland.

Miikka Mwamba pia ndiye ametengenezwa wimbo wa K Sal ‘Mwana Mkiwa’ akimshirikisha Q Chief. Mwaka 1993 ndipo Miikka alikuja nchini, kati ya 1990 hadi 2000 alifanya kazi FM Studio na kutengenezwa nyimbo nyingo kubwa za Bongofleva.