Mtitu alia na filamu kushushwa bei

Muktasari:
Mtitu alisema hizo ni hila za wazi za kuua kampuni nyingine ndogondogo ili kampuni hiyo ibaki peke yake.
MSANII na Mwongozaji wa filamu Swahilihood, William J. Mtitu amesema hawatakuwa tayari kuona familia zao zikifa kwa kukosa mahitaji kufuatia kampuni moja kuamua kushusha bei ya filamu kutoka Sh3,000 hadi 1,500.
Mtitu alisema hizo ni hila za wazi za kuua kampuni nyingine ndogondogo ili kampuni hiyo ibaki peke yake.
“Maisha kila siku yanapanda, sasa mkate unauzwa Shilingi 3,000, halafu mtu mmoja mwenye fedha zake anataka kuua familia za Watanzania wanaojishughulisha na kazi za kusambaza filamu kwa kushusha bei, si ana mpango wa kutuua huyo? Hatutakubali,”alisema.
Mtitu anasema historia inaonyesha kuwa tangu kuingia kwa kampuni hiyo katika usambazaji, kampuni nyingi zimekufa baada kila msimu kushusha bei na hali hiyo bado inaendelea.
Moja ya sababu kubwa ya kushusha bei inasemekana ni kutokana na maharamia kutawala soko hilo na kushindwa kushughulikiwa ipasavyo.