Mjukuu wa Bob Marley afanya kufuru

Muktasari:

  • Wimbo huo uliongezeka umaarufu baada ya binti wa Kim Kardashian na Kanye West aitwaye North West alipoutumia wimbo huo katika video yake ya TikTok, ambayo iliangaliwa mara milioni 30.

UNAWEZA kuita hii ni kufuru kwa mambo anayoyafanya mjukuu wa Bob Marley tangu aachie ngoma yake ya ‘Praise Jah in the Moonlight.’ YG, ambaye ni mtoto wa Lauryn Hill na Rohan Marley, ameitingisha dunia kutokana na ngoma yake hiyo kufanya vizuri sana kila mahali.

Akiwa na umri wa miaka 22 tu, YG kupitia wimbo wake wa ‘Praise Jah in the Moonlight,’ ameandika historia kwa kuwa wimbo wa kwanza wa reggae kufikisha streams bilioni 1 duniani kote.

Wimbo huo ambao ameuandika kwa kushirikiana na mama yake, Lauryn Hill, umepata mafanikio makubwa katika streaming za mitandao, zilizoufanya ufike hadi Na. 34 katika chati za Billboard Hot 100.

YG akitumbuiza na mama yake Lauryn Hill

Mchango wa Lauryn Hill katika wimbo huo, kuanzia mashairi na hadi kurekodiwa, umetambuliwa na mashabiki wake ukitajwa kuwa moja ya sababu za mafanikio ya jumla ya wimbo huo. Lauryn Hill ambaye alitamba na kundi la Fugees miaka ya 1990 akiwa na  wanamuziki wenzake wa Wyclef Jean na Pras, ameshiriki kidogo katika video ya mwanaye huyo ya wimbo ‘Praise Jah in the Moonlight’.

“Praise Jah in the Moonlight” uliachiwa Desemba 27, 2023, lakini ukaanza kubamba mwishoni mwa Januari na mwanzoni mwa Februari 2024.

Mwezi Machi, wimbo huo ukatinga katika Top 10 ya TikTok Billboard Top 50 na kushika Na.2 baada ya kubamba sana katika mitandao ya kijamii. Wimbo huo ni sampo ya wimbo “Crisis” wa Bob Marley na kundi lake la The Wailers.

Wimbo huo uliongezeka umaarufu baada ya binti wa Kim Kardashian na Kanye West aitwaye North West alipoutumia wimbo huo katika video yake ya TikTok, ambayo iliangaliwa mara milioni 30. Staa wa Internet, Leah Halton aliposti video akiuimba kwa kufuatisha mashairi katika  TikTok, ambayo ikawa moja ya video maarufu zaidi katika mtandao huo imetazamwa mara milioni 776.6 na ikapata ‘likes’ milioni 49.5 kufikia leo.

Lauryn Hill na Wyclef Jean wakimpa sapoti YG Marley

YG Marley amekuwa akifanya ziara mbalimbali za maonyesho akiwa na mama yake ikiwamo kutumbuiza Jamaica na Marekani.

YG Marley, ambaye jina lake halisi ni Joshua Omaru Marley, ni kati ya kizazi cha tatu cha Marley ambao wanaendelea kuwasha katika muziki. Wakati wa sherehe ya bethidei ya Jo Mersa Marley, nyota kadhaa wa kizazi kipya cha Marleys walioanda stejini kutumbuiza akiwamo motto wa Damian “Jr. Gong” Marley, Christian Marley, Mystic Marley, Zuri Marley, na Yohan Marley. Marafiki wa familia katika muziki wa reggae kama Buju Banton, Sizzla Kalonji, Capleton, Spragga Benz, na wengine wengi walihudhuria na kutumbuiza.

Muziki wa Bob Marley pia umeuzika sana kupitia ‘streaming’ ya mtandaoni katika wiki kadhaa zilizopita soko ambalo limeamshwa na mafanikio ya filamu ya maisha ya Bob Marley: One Love biopic.

YG Marley akiwa na mama yake, Lauryn Hill na baba yake, Rohan Marley

wa mujibu wa Box Office Mojo, filamu hiyo imeongoza kwa kuingiza Dola 89 milioni katika US box office kufikia Machi 10, 2024, na jumla imeingiza Dola 160 milioni duniani.

Mijadala ni mingi kwamba wimbo wa YG wa ‘Praise Jah in the Moonlight,’ ulipaswa kuwania tuzo ya Grammy ya Wimbo Bora wa Mwaka.

Sehemu ya mashairi ya wimbo huo ambao ndio wimbo wa reggae unaotingisha dunia kwa sasa yanasema:

“Wanasema jua linawamulikia wote,

Lakini kwa baadhi ya watu duniani haliwapi chochote,

Hii miale yote inawaka moto, ahh

Kuonyesha kwamba nilikupenda, lakini bado unaniita mwongo.

Oh, no, no, no, no, no…”

MASHAIRI KAMILI

Wimbo: Praise Jah In The Moonlight

Msanii: YG Marley

They say the sun a na shine for all

But in some people world

It never shine at all

These roads of flames are catching a fire, ahh

Showed you I loved you, and you called me a liar

Oh, no, no, no, no, no

Baby, tell me where you gone, gone, gone

I've been fiendin' for your love so long

We can praise Jah in the moonlight

Baby, if you with me better do right

And I've been gone too long

And I'm hoping that you sing my songs (sing my songs)

I've been on this road for way too long

I've been hoping that we all get along

These roads of flames are catching a fire, ahh

Showed you I loved you, you called me a liar

Give Jah the thanks and praises

I've been on my own all along

But we ain't never left alone, 'lone, 'lone

And if I'm telling you the feeling is wrong

Relax a little, friend, this won't take too long

And when you're feeling alone

You can call my phone

Is there a better way to go?

Teach them something before they lose their soul

Oh, no, no, no freedom is the road

Oh, no, no, no coming in from the cold

Tell them not to sell it, it's worth more than gold

And guiltiness will catch them in the end

Oh yeah, oh yeah

They'll try to manipulate you through your pockets (ahh)

Now you're caught up in a funk with the optic, with the vision (ahh)

Trying to control your soul and take control

Oh, no, no, no (ahh)

No, we don't play that game right here to win power (ahh)

Give Jah the thanks and praises

(Give Jah all the thanks and praises) give Jah the thanks and praises

(Give Jah all the thanks and praises) I sing, give Jah the thanks and praises

(Give Jah all the thanks and praises) give Jah the thanks and praises

(Give Jah all the thanks and praises) give Jah the thanks and praises

(Give Jah all the thanks and praises) give Jah the thanks and praises

Oh, give Jah all the thanks, the thanks

The thanks, the thanks, the thanks (give Jah thanks and)

The thanks, thanks, thanks, thanks, thanks (praises)

Thanks, thanks, thanks, thanks, thanks and praises (praises)

(Give Jah thanks and)

Give Jah the thanks and praises (praises, praises)

(Give Jah thanks and praises, praises)

(Give Jah thanks and praises, praises)

(Give Him the thanks and the praises)