Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maunda Zorro kuzikwa Jumamosi Kigamboni

Dar es Salaam. Mwili wa Msanii Maunda Zorro unatarajiwa kuagwa na kuzikwa siku ya Jumamosi Aprili 16 eneo la Toangoma, Kigamboni.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Aprili 14, 2022 na baba yake Zahir Zorro, alipozungumza na Mwananchi.

Zorro ambaye ni mwanamuziki wa siku nyingi, amesema shughuli zote za msiba zitafanyika nyumbani kwake Maweni na atazikwa kwa dini ya kikristo.

"Maunda niliridhia abadili dini na alibatizwa tangu akiwa na mwaka mmoja hivyo ni mkristo na atazikwa kwa dini hiyo" amesema Zorro.

Akielezea namna alivyopata taarifa za msiba amesema aliipata saa kumi za usiku, baada ya mtoto wake wa Banana Zorro kumpigia, licha ya kuwa tayari alikuwa kashapata tetesi kuwa alipata ajali lakini hakuwa na uhakika kwamba amejeruhiwa au amefariki.

Enzi za uhai wake Maunda aliwahi kutesa na nyimbo mbalimbali ikiwemo Mapenzi ya Wawili,Nataka Niwe wako na nyingine nyingi.

Maunda amefariki akiwa ameacha watoto watatu.