Matano yaliyomvutia Jux kumuoa Priscilla

Muktasari:
- Jux alifunga ndoa ya Kiislam na Priscilla Ojo, Februari 7, 2025 jijini Dar es Salaam kisha wakaenda kufanya sherehe Nigeria kabla ya Jumatano iliyopita kufanya sherehe nyingine jijini Dar es Salaam na Mwanaspoti lilimbana kutaka kujua kilichomvutia kwa bibie huyo Mnigeria naye kufunguka.
MKALI wa miondoko ya R&B nchini, Juma Jux ameendelea kutrendi baada ya kufanya sherehe ya mwisho ya harusi yake na Priscilla Ojo wa Nigeria, huku akiamini mambo matano yaliyochangia kuangukia kwa kimwana huyo.
Jux alifunga ndoa ya Kiislam na Priscilla Ojo, Februari 7, 2025 jijini Dar es Salaam kisha wakaenda kufanya sherehe Nigeria kabla ya Jumatano iliyopita kufanya sherehe nyingine jijini Dar es Salaam na Mwanaspoti lilimbana kutaka kujua kilichomvutia kwa bibie huyo Mnigeria naye kufunguka.
Jux alisema kwa mwanaume yeyote akimtokea mtu, ni lazima awe na vigezo vilivyochangia kujitosa kwa bibie naye alisema kuna mambo matano yaliyochangia kumzimia Priscy.
“Mambo matano yaliyonivutia kwa huyu hadi kumuoa ni haya, kwanza ni vile sikutaka kuoa mwanamke ambaye ana mtoto, sababu mimi katika maisha yangu sikutaka kupata mtoto nje ya ndoa, hivyo kutokuwa na mtoto ilikuwa kigezo cha kwanza, pili ana upendo, ni msomi, nne ni mfanyabiashara na mwisho ni kwa vile ni mzuri Mash’Allah,” alisema Jux.
Pia Jux alisema ni kawaida kwa wana ndoa baada ya kufanikisha jambo hilo, kinachofuata ni kutafuta mtoto na analiacha hilo mikononi mwa Muumba.