Mama Diamond: Mlitakaje? Nassibu ndo keshaoa!

Muktasari:
- Mama Dangote amekuwa akihusishwa sana na ishu ya kupendana ama kutibuana baina ya mastaa hao wawili wa muziki wanaofanya kazi pamoja katika lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).
Hatimaye mama mzazi wa msanii Diamond Platnumz, Sanura Kassim aka Mama Dangote amevunja ukimya na kuanika juu ya ndoa ya mtoto wake na Zuchu, baada ya uvumi wa mastaa hao kuoana ama kutalikiana kutawala mitandao ya kijamii.
Mama Dangote amekuwa akihusishwa sana na ishu ya kupendana ama kutibuana baina ya mastaa hao wawili wa muziki wanaofanya kazi pamoja katika lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).
Akizungumza na Mwanaspoti, Mama Dangote amesema anawashangaa watu wanaoshangazwa na taarifa juu ya Diamond kuoa akihoji kwani walitakaje? Maana siku zote watu humsema mitandaoni kuwa aoe na sasa ndio keshaoa.

"Kabla ya hiyo taarifa ya ndoa, yalisemwa mengi kuhusu Nassibu, sasa watu walitakaje? Nassibu ndio keshaoa hivyo, maana naona watu wengi leo ni full kuchanganyikiwa kila mmoja anasema yake (kicheko)," amesema Mama Dangote.
Mwanaspoti lilimuuliza imekuwaje naye Mama Dangote ampe pongezi Diamond kama vile naye amelifahamu jambo hilo jana ikiwa ni kweli Mondi alishaoa siku nyingi kama staa huyo mwenyewe alivyoandika katika posti yake, mama huyo akasema:
"Sasa hapo muoaji ni Diamond na yeye ndio ameliweka wazi jana kwahiyo hata comment zinatakiwa zegemee jana hiyo kuhusu alichoposti, kwanza mimi sitaki maswali mengi bwana nina shughuli zangu nafanya hapa nipigie baadaye," amesema.
Jana usiku Juni 1, 2025 Diamond Platnumz aliweka wazi kuwa aliwahi kufunga ndoa ma mpenzi wake ambae pia ni msanii wake Zuchu.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram ameandika…
"Miongoni mwa vitu ambavyo nimejifunza ni ukomavu wa kukaa kimya... ukomavu huu unataka uvumilivu wa hali ya juu, inataka uwe na moyo wa subra na hasa kukaza roho pindi mtu au watu wanapokuwa wanakupakazia ubaya fulani kwenye jamii halaf wewe una ukweli wake lakini unatakiwa ukae tu kimya usijibu ilhali ukweli unao ndani...Kwakweli si jambo jepesi linataka ustahmilivu wa hali ya juu sana, na siwezi sema eti nauweza sana, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu amenijaalia hekima hiyo kwa kiwango chake, na nimekua nikiishi hivyo kwa muda mrefu kukaa kimya pindi yoyote akijaribu kusema lolote dhidi yangu, na ndio maana hata interview nimekuwa naepuka kufanya siku hizi... japo si jambo jepesi lakini faida yake nimeiona na ni kubwa maana vita vyako inakuwa unapambaniwa na Mwenyezi Mungu na inakufanya uwe Mmshindi kila siku....

"Anyways: Najua kila mmoja wenu ana picha tofauti kabisa kuhusu Diamond Platnumz na KUOA, ila tu nataka leo niwaambie kuwa HUYU DIAMOND PLATNUMZ ALISHAWAHI KUOA, na kuna siku nitawaambia ikawaje."
Kauli kwamba "Diamond alishawahi kuoa" imetafsiriwa na wengine kuwa huenda uvumi wa kumtaliki Zuchu ukawa na ukweli.