Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shekhe Walid akiri kuwafungisha ndoa Diamond, Zuchu

WALID Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Shekhe Walid amesema aliwafungisha ndoa hiyo wanamuziki hao miezi mitano iliyopita, lakini habari za kuachana hazifahamu.

Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Kawambwa amesema kwamba alifungisha ndoa Diamond Platnumz na Zuchu miezi michache iliyopita.

Akizungumza na Mwanaspoti, Shekhe Walid amesema aliwafungisha ndoa hiyo wanamuziki hao miezi mitano iliyopita, lakini habari za kuachana hazifahamu.

"Kwanini watu wanapenda watu wengine wazini? Diamond na Zuchu ni kweli nimewafungisha ndoa mimi toka miezi mitano iliyopita, ila hilo swali lako unaloniuliza kuhusu wameachana mimi silifahamu sababu kama wangekuwa wameachana Diamond angekuja kuniambia," amesema Shekhe Walid.

"Vile mlivyoona kwenye mitandao ni kweli ndoa wala sio kiki, ila naona watu wengi wameshtushwa na hii habari maana mmezoea kuwasemasema Diamond na Zuchu wazini kila kukicha sasa hili jambo la heri lishangilieni na kuliombea heri."

Shekhe Warid hakutaka kuzungumzia hatua zilivyoanza hadi akatafutwa kuwafungisha ndoa Diamond na Zuchu na kwanini ilikuwa siri.

"Mimi sitaki kuzungumzia chochote kile, swali lako nishakujibu kuwa kweli wamefunga ndoa. Hayo mambo mengine ya kiundani zaidi sio jukumu langu kuwaelezea," amesema.

Naye Khadija Kopa, mama wa Zuchu, leo Mei 3, 2025 akizungumza na Mwanaspoti ametoa sababu kwanini hakuhudhuria ndoa hiyo.

'Mimi kama nilivyosema jana ndoa ni jambo la heri. Zuhura ameolewa na Diamond japo walifanya siri, lakini ni jambo la heri," amesema mzazi huyo.

"Kuhusu kutohudhuria kwenye ndoa sisi kama wazazi yaani mimi na baba yake Zuhura tulishatoa ruhusa kama akitaka kufunga ndoa, basi afunge tu hata kama sisi hatutakuwepo kiufupi tulitoa baraka zote kwa mtu yeyote atakayempata, na vizuri kampata mtu wamefunga ndoa kisirisiri, yote heri.

"Nimeona kuna watu wanasema kwanini Shekhe Walid amemshika mkono Diamond na sio baba yake Zuhura. Unajua sisi kama sisi Waislamu wakati wowote shekhe wetu anaweza kuwa Walii kwa upande  wa mtoto, na sisi tulishatoa ruhusa kwa Shekhe Warid kuwa ndio baba yake wa hapa anayemsimamia.

"Hivyo wakati wowote akiwa na jambo la ndoa kwa mtu yeyote Zuhura aende tu kwa Shekhe Warid. Na kingine mimi Zuhura nilimzaa nikiwa siko kwenye ndoa, hivyo kama kuozeshwa angeozeshwa na kaka yake."