Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marioo, Paula waonyesha sura ya mtoto wao kwa mara ya kwanza

Muktasari:

  • Mtoto huyo ambaye leo ametimiza mwaka mmoja, mashabiki wamepata fursa ya kuiona sura yake baada ya Marioo na Paula kumposti katika akaunti zao za Instagram.

Mashabiki wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo na mpenzi wake, Paula walikuwa wanasubiri kwa hamu kuiona sura ya mtoto wa kwanza wa mastaa hao aitwaye Amara ambaye toka amezaliwa alikuwa akifichwa.

Mtoto huyo ambaye leo ametimiza mwaka mmoja, mashabiki wamepata fursa ya kuiona sura yake baada ya Marioo na Paula kumposti katika akaunti zao za Instagram.

Akizungumza na Mwanaspoti kuhusu kuficha sura ya mtoto wao, Paula amesema: "Kiukweli mimi niseme tu nilikuwa napenda mwanangu aonekane mapema sura yake baada ya hapo ndio asionekane kwenye mitandao hadi atakapojitambua, ila baba yake hakutaka hivyo na mimi nikakubaliana naye.

"Niliona jambo zuri mtoto mdogo sura yake isikae kwenye mitandao, bora akue vizuri kwanza kama hivi alivyotimiza mwaka mmoja ndio aonekane."

Kwa upande wa Marioo, amesema: "Kwanza namshukuru Mungu kwa mtoto wangu kutimiza mwaka mmoja, tukija kwenye sababu kwanini nilimficha sura nilitaka kwanza achangamke na pia haya mambo ya Instagram ni maisha ambayo siyataki watu wayazoee kwa mwanangu.

"Utaonyesha sura leo, kesho sura hiyohiyo itaanza kutumika vibaya kwenye baadhi ya kurasa za udaku, hivi kwa leo kutimiza mwaka mmoja na kuonyesha sura yake haitakuwa kila wakati anaonekana mitandaoni."

Marioo amesema katika kusherehekea mtoto wao kutimiza mwaka mmoja, leo usiku watamfanyia sherehe ya pongezi na kualika wageni mbalimbali.