Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUONGEE KISHKAJI: Tumpandishe Dogo Pateni bila kumshusha Dogo Sajenti

Muktasari:

  • Umeshasikia ule wimbo wa singeli unaimbwa “Ibilisi alinipanda sa’ ningefanya nini, nilijikuta najitetea sababu nina panga kiunoni, ila afande, sio kama nauza mwenyewe nauzia, ile kesi ya robari afande nimesingiziwa, afande n’legezee kamba ili niweze kukupanga afande.”

MSANII aliyetrendi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii wiki hii anaitwa Dogo Pateni. Ni msanii wa singeli ambaye hata kama humfahamu, basi utakuwa unajua moja ya kazi zake maarufu.

Umeshasikia ule wimbo wa singeli unaimbwa “Ibilisi alinipanda sa’ ningefanya nini, nilijikuta najitetea sababu nina panga kiunoni, ila afande, sio kama nauza mwenyewe nauzia, ile kesi ya robari afande nimesingiziwa, afande n’legezee kamba ili niweze kukupanga afande.”

Basi Dogo Pateni ndo kaimba wimbo huo. Najua anatrendi Dogo Pateni, lakini nataka tusimuongelee yeye. Nataka tumuongelee msanii mwingine wa singeli anayeitwa Dogo Sajenti.

Sajenti na Pateni walikuwa ni wasanii wanaoimba pamoja. Hawakuwa kundi walikuwa wanaimba pamoja tu. Walipoanza kwenda ‘viral’ menejimenti ikaanza kuwazingitia kwenye uwekezaji. Wakaanza kuwalipia pesa za video kali - miksa - kuwanunulia pamba kali za kushutia vichupa.

Lakini wakati hayo yanaendelea, Pateni akaanza kulalamika kwenye mitandao ya kijamii kwamba menejimenti ni kama inafanya upendeleo. Pamba kali wanamnunulia Sajenti peke yake, kwenye shoo wanampeleka Sajenti peke yake wakidai kwamba eti wateja wanataka msanii mmoja ambaye ndo huyo Sajenti.

Basi malalamiko ya Pateni yakawafikia Watanzania wa mitandaoni na walichokifanya ni kuanza kumuonyesha shoo Sajenti. Wakaanza kukomenti vibaya kwenye posti za Sajenti na kuanza kumtrendisha Pateni ambaye alikuwa analalamika ananyanyaswa. Na kweli, kufumba na kufumbua Pateni akawa staa kuliko unavyodhani na hivi ninavyokwambia ana ngoma amefanya na Zuchu wa WCB Wasafi.Kwanini nataka tumuongelee Sajenti? Ni kwa sababu Watanzania hatumtendei haki huyu dogo.

Sasa hivi kila anachoposti kwenye mitandao yake ya kijamii anaambulia matusi, komenti mbaya, kusimangwa kwamba hajui kuimba na kuchekwa kwamba amefeli wakati mwenzake anapasua anga. Kwa kifupi, Dogo anafanyiwa uonevu mkubwa sana. Kimombo wanaita ‘bullying’. Na mbaya zaidi Sajenti bado mdogo sana sidhani hata kama umri wake unaruhusu kupiga kura mwaka huu. Na mtoto mwenye umri mdogo kama Sajenti hana uwezo wa kumudu maumivu ya kihisia anayopewa na komenti za Watanzania.

Kuna video nimeona Sajenti anaongea kwa huzuni jinsi anavyofanyiwa na Watanzania, anasema “watu wanakomenti wanasema sijui kuimba. Inanikatisha tamaa hata ya kuendelea kufanya muziki.” Maneno kama hayo sio dalili nzuri kutoka kwa mtu mwenye umri wa Sajenti.

Tunachokifanya sasa ni kumsukumia kwenye matatizo. Tunampa msongo wa mawazo mdogo wetu - msongo ambao baadaye anaweza kuutumia kama sababu ya kuanza kujihusisha na mambo mabaya na tutakuwa tumepoteza kipaji mapema sana. Hakuna haja ya kumshambulia Sajenti kwani hata tuhuma hazikuwa za kwake - zilikuwa za menejimenti.

Tuache hii tabia ya kulazimisha kumshusha mmoja ili kumpandisha mwingine. Keki ya sanaa ni kubwa sana tungeweza kuwalea Pateni na Sajenti kwa pamoja ili tasnia iendelee kuwa na wasanii wakali kwani kwa kusema ukweli hawa madogo wote wawili wana vipaji vikubwa.