Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marioo na Mimi Mars kama Mondi na Wema tu!

NI kipaji kingine kilichonolewa Tanzania House Talent (THT), mwaka 2018 ndipo Marioo aliachia ngoma yake, Dar Kugumu iliyomtoa kimuziki lakini ilikuwa imerekodiwa tangu mwaka 2015, wazo la kuandika wimbo huo lilimjia kutokana na kazi aliyokuwa anaifanya ya gereji.

Hadi sasa Marioo ametoa ngoma nyingi zilizofanya vizuri pamoja na albamu moja, The Kid You Know (2022), ameshinda tuzo tatu za Tanzania Music Awards (TMA) 2021, huku Abbah akiwa ndiye Prodyuza aliyetengeneza ngoma nyingi zake. Songa nayo; 

1. Kipindi Aslay anatoka na ngoma yake, Nakusemea ambayo ilibeba jina la albamu yake ya kwanza, alimvutia Marioo na kuona inawezekana kutoka kimuziki katika umri mdogo tu, ndipo naye akaanza harakati za kuingia katika muziki wa Bongofleva.

2. Marioo aliwahi kulia machozi mbele ya Dully Sykes baada ya kupigiwa simu na Mama yake mzazi na kumtaka kuachana na muziki na ajikite kwenye kazi ya kuchomelea (gereji) kwani muziki hauwezi kumlipa.

Na aliamua kuondoka nyumbani baada ya kutakiwa kuacha muziki, akawa anafanya kazi na Prodyuza Abbah hadi kulala studio kwake na kufanya usafi, nyimbo zake mbili za mwanzo kurekodi kwa Abbah ni Mboni Yangu na Dar Kugumu.

3. Prodyuza Bonga ambaye ametengeneza wimbo wa Harmonize 'Uno' na nyinginezo, alikuwa anaishi Ghetto moja na Marioo kabla ya kutoka kimuziki, Bonga ni miongoni mwa watu waliomsaidia sana Marioo kutokana hakuwa na uwezo wa kulipia studio.

4. Siku ambayo Marioo anakutana na Nandy studio kwa mara ya kwanza ili kumwandika wimbo, alikuwepo Prodyuza Lollipop (Goodluck Gozbert) ambaye ameandika nyimbo kibao zilizofanya vizuri kama Moyo Mashine ya Ben Pol, Basi Nenda na Mo Music n.k.
Uwepo wa Lollipop studio uliondoka ujasiri wa Marioo, hivyo aliomba kupewa mdundo aende nao nyumbani kuandika, alipomaliza kesho yake na kumtumia Nandy alikubali uwezo wake na ukawa mwanzo wa kufanya kazi pamoja.

5. Wimbo 'Wasikundanganye' ambao Marioo kamwandikia Nandy, tayari alikuwa ameshaurekodi kwa Bonga, walipokuwa ndani ya gari wakienda studio kwa Kimambo, ndipo Nandy akaupenda na kumuomba aurudie huo, baada ya hapo historia ikaandikwa.

6. Baada ya kufanya cover ya wimbo wa Ditto, Moyo Sukuma Damu ndio milango ilianza kufunguka kwa Marioo, Prodyuza Yogo aliipenda cover hiyo akaichukua na kwenda kuifanyia 'mixing'  vizuri.
Prodyuza Emma The Boy naye aliposikia cover hiyo akaikubali hadi kumueleza Bosi wa THT, Marehemu Ruge Mutahaba kuhusu uwezo wa Marioo na huo ukawa mwanzo wa kupata nafasi THT, huku akiendelea kufanya kazi na Abbah.

7. Marioo amewaandika nyimbo wasanii kama Nandy (Wasikudanganye), Christian Bella (Pambe), Gigy Money (Papa),  Dogo Janja (Banana), Lyyn (Chafu), Shilole (Mchakamchaka), Mwasiti (Bado), Amber Lulu (Jini Kisirani), Ditto (Nabembea) n.k.

8. Katika miaka miwili iliyopita, Marioo ameshirikishwa kwenye nyimbo zaidi ya 20, mmoja wapo ni 'Loyalty' wake Darassa kutoka kwenye albamu yake, Slave Becomes A King (2020) ulioshinda tuzo ya TMA 2021 kama Wimbo Bora wa Kushirikiana.

9. Marioo ndiye msanii wa kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kufikisha 'streams' milioni 100 katika mtandao wa Boomplay Music bila kuwa na albamu wala EP. Wakati Rayvanny, Diamond Platnumz, Zuchu, Mbosso na Otile Brown kutokea Kenya walifanya hivyo wakiwa na albamu au EP.

10. Mimi Mars ni miongoni mwa Walimu waliomfundisha Marioo aliyeishia kidato cha pili lugha ya Kiingereza, pia huyu ndiye msanii wa kike Bongo aliyemshirikisha zaidi Marioo katika ngoma zake, mbili, La La na Una ambao pia Young Lunya alipewa shavu.
Hiyo ni sawa na Wema Sepetu ambaye alimfundisha Diamond Platnumz Kiingereza kipindi wana uhusiano, Wema, Miss Tanzania 2006, ndiye mrembo Bongo aliyetajwa zaidi kwenye ngoma za Diamond kama Nimpende Nani, Kesho, Fire n.k.