Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbosso azindua EP, afya yake yaibua simanzi

MBOSSO Pict

Muktasari:

  • EP hiyo iliyoshuhudiwa na watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa Bongo fleva, nyimbo za Injili, Taarabu, Singeli na wasanii wa maigizo, ilijaa furaha, simanzi na vilio baada ya Mbosso kupanda jukwaani kuielezea kazi yake hiyo yenye nyimbo sita  ambazo ni Pawa, Nusu Saa, Tena, Merijaah, Siko Single na Aviola sambamba na Bonus Track aliyoiita Asumani.

UKIMYA wa muda mrefu aliokuwa nao mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mbwana Yusuph 'Mbosso' tangu atoke Lebo ya WCB, umezaa matunda baada ya usiku wa Juni 12, 2025 kuzindua EP aliyoipa jina la 'Room  Number 3', tukio likifanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

EP hiyo iliyoshuhudiwa na watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa Bongo fleva, nyimbo za Injili, Taarabu, Singeli na wasanii wa maigizo, ilijaa furaha, simanzi na vilio baada ya Mbosso kupanda jukwaani kuielezea kazi yake hiyo yenye nyimbo sita  ambazo ni Pawa, Nusu Saa, Tena, Merijaah, Siko Single na Aviola sambamba na Bonus Track aliyoiita Asumani.

SIKU MBILI KABLA YA SHOO AKIMBIZWA HOSPITALI
Alipopanda jukwaani, Mbosso alianza kuelezea kuwa siku mbili kabla ya kufanyika kwa uzinduzi huo, aliumwa sana na kupelekwa hospitali, hivyo alikuwa na hofu kubwa juu ya kinachomsumbua. Taarifa hii ilitia simanzi na ukumbi mzima ulikuwa kimya ghafla kwa takribani dakika tatu.

"Unajua kuandaa kitu kama hiki yataka ujasiri sana, hamuwezi kuamini mimi niliumwa siku mbili kabla ya huu uzinduzi wa EP yangu ambapo nikakimbizwa hospitali nikaambiwa nimepatwa na  mchafuko wa damu. Mwanzo niliogopa nikadhani tatizo langu la moyo limerudi.

AELEZEA MAANA YA ROOM NUMBER 3, AMPA MAUA YAKE ASLAY 
Mbosso amefafanua sababu za EP hiyo kuitwa Room Number 3 ambapo alianza kwa kueleza hivi;

"Hii ni safari yangu ya ukuaji ya maisha ya kimuziki, hivyo Room Number 1 ni chumba ambacho tulikimaliza kwa muda mrefu, ni chumba ambacho nakishukuru sana kwenye maisha yangu ya muziki, kwa sababu kilinitambulisha kwa watu wote ambao walikuwa hawamjui Mbosso, hivyo shukran nyingi kwa Mkubwa Fella kwa wakati huo nipo Yamoto Band.

"Lakini pia naomba mumpigie makofi mengi ya shukurani msanii mwenzangu Aslay, nimemtaja Aslay kwa sababu kipindi naanza muziki, siku yangu ya kwanza kuwa msanii wa Mkubwa na Wanawe  ni kwasababu nilimuona Aslay anaimba.

"Tukiwa pale kituoni, nikamsikia Mkubwa Fella anasema anahitaji vijana rika kama la Aslay wenye uwezo wa kuimba kama yeye, kwa hiyo kupitia Aslay nilipata ujasiri wa kuamini kumbe na mimi naweza kuimba, hivyo basi Aslay ndiye aliyenishawishi kuingia kwenye muziki pia kupitia yeye nilijifunza vitu vingi sana mpaka leo hii kuwa hapa.

"Room Number 2 yalikuwa maisha mazuri sana kwangu, ya furaha, upendo na kupata marafiki ambao tulikuwa tumeshibana sana na vijana wenzangu ambao wote tulikuwa tunaiunganisha Lebo ya Wasafi ambao ni Diamondi Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Queen Darling, Rich Mavoko, Lavalava, hadi tukaja kumpata Zuchu na D Voice.

"Kwa hiyo Room Number 2 niliona utamu wa sukari wa muziki wangu, nilipata mafunzo makubwa sana, nilionana na matajiri wengi, watu maarufu wengi, na kukutana na viongozi wa ngazi za juu, kwa hili namshukuru sana Diamond Platnumz kwa sapoti kubwa aliyonipa.

"Room Number 3 ndio imetufanya tuwe hapa leo, chumba hiki kina stori nyingi za maisha ya furaha na upendo, imenichukua takribani miezi minne au mitatu kwa ajili ya kutengeneza kitu kizuri kwa watu wanaonisubiri muda mrefu juu ya kazi zangu, unajua kuna wengi wao mapenzi yao yananizidia, hivyo nilikuwa nawaamgusha, lakini ilikuwa sio kitu cha kufanya haraka, hivyo nilikuwa naandaa kitu kizuri kwa ajili ya watu wangu hata wale ambao sio wangu niwafanye wawe wangu. Leo tunaanza safari ya chumba namba tatu kwa kusikiliza EP yangu yenye nyimbo 6," amesema Mbosso.

VILIO 
Baada ya uzinduzi, Mbosso alipanda jukwaani kwa kuwashukuru watu waliohudhuria ukumbini hapo, lakini kabla ya kushuka, mshehereshaji wa tukio hilo, mtangazaji Lil Ommy alimwambia aimbe wimbo hata mmoja uliopo kwenye EP kwa ajili ya mashabiki wake waliohudhuria.

Mbosso akachagua wimbo wa 'Pawa' uliomfanya Queen Darling katikati ya wimbo huo kupanda jukwaani na kumkumbatia, wakaanza kulia, jambo lililomfanya Mbosso kushindwa kuendelea kuimba, wakashuka.

FURAHA 
Wakati Dj akipiga kila wimbo uliokuwa kwenye EP, nusu ya ukumbi walikuwa wanainuka kucheza na wengine kupanda juu ya jukwaa kucheza na Mbosso.

ATOA SHUKURANI
Aidha Mbosso amesema, Room Number 3 inapatikana kwenye majukwaa yote ya kusikiliza muziki, huku akiwashukuru pia Watanzania wote kwa kuendelea kuwa naye katika jitihada zake za muziki.

Amesema ndani ya EP yake imebeba mafunzo mengi yenye kufundisha na kuelimisha, hivyo amewataka mashabiki kuendelea kumpa ushirikiano wa kutosha katika kuipakua EP hiyo.