Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madee kutambulisha wasanii wake wawili mwaka huu

Muktasari:

  • Hata hivyo alisema lebo hiyo haihusiani na Tip Top isipokuwa itakuwa inajisimamia yenyewe na kueleza kuwa amepania kuinua vipaji vya vijana wenye ndoto za kutoka kwenye muziki.

Kasi ya wasanii wa zamani kuwa na wasanii wao inazidi kushika chati, na mara hii msanii kutoka Manzese, Hamadi Seneda maarufu kwa jina la Madee anatarajia kutambulisha wa kwake wawili kupitia lebo yake ya Manzese Music.

Katika mahojiano maalum na Mwananchi alisema tayari mwaka jana walimtambulisha Gaza aliyetoa naye wimbo wa ‘Nanii ‘.

Hata hivyo alisema lebo hiyo haihusiani na Tip Top isipokuwa itakuwa inajisimamia yenyewe na kueleza kuwa amepania kuinua vipaji vya vijana wenye ndoto za kutoka kwenye muziki.

Wasanii wengine ambao kwa sasa wanamiliki wasanii mbali na Madee ni pamoja na Shetta anayewasimamia bendi ya The Mafik, Ali Kiba na lebo ya KingsKiba na Diamond na lebo ya WCB