Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maajabu ya binti wa Beyonce na Jay Z

Muktasari:

  • Huyu Blue Ivy naye ni mshindi wa Grammy, tuzo aliyoshinda akiwa na umri wa miaka tisa tu kupitia wimbo, Brown Skin Girl (2021) ambao alishirikishwa na mama yake Beyonce, hivyo kuandika rekodi kama mtu mdogo zaidi wa pili duniani kufanya hivyo. 

HIVI karibuni katika tuzo za Grammy 2025, miongoni mwa wageni walihudhuria na kuangaziwa sana na vyombo vya habari ni pamoja na binti wa kwanza ya Beyonce na Jay Z, Blue Ivy Carter, 13, ambaye anafanya muziki pia.

Huyu Blue Ivy naye ni mshindi wa Grammy, tuzo aliyoshinda akiwa na umri wa miaka tisa tu kupitia wimbo, Brown Skin Girl (2021) ambao alishirikishwa na mama yake Beyonce, hivyo kuandika rekodi kama mtu mdogo zaidi wa pili duniani kufanya hivyo. 

Je, binti huyo wa Beyonce ana maajabu gani katika tasnia ya burudani? Blue Ivy alizaliwa Januari 7, 2012, New York, Marekani anatajwa kuwa ni mtoto maarufu zaidi duniani baada ya Prince George kutoka familia ya Kifalme ya Uingereza.

Beyonce alipotangaza kuwa na ujauzito wa Blue Ivy hapo Agosti 28, 2011 wakati akitumbuiza katika tuzo za MTV VMAs, tangazo hilo lilivunja rekodi duniani katika mtandao wa X (zamani Twitter) kwa kupata tweet 8,860 kila sekunde. 

Na baada ya kuzaliwa tu sauti yake ilisikika kwenye wimbo Glory (2011) wa Jay Z ambao uliingia katika chati za Billboard na kumfanya Blue Ivy kuandika rekodi nyingine ya dunia kama mtu mdogo zaidi kuingia kwenye chati hizo.

Hata hivyo, aliposikika katika wimbo 'Brown Skin Girl' kutoka kwenye albamu ya Beyonce, The Lion King: The Gift (2019) akishirikisha wasanii wengine Saint JHN na Wizkid, ndio ulimpatia mafanikio makubwa zaidi kimuziki.

Kupitia wimbo huo alishinda tuzo 10 kuanzia Grammy, MTV VMAs, Shorty, The Daily Califonian, Soul Train (2), NAACP Image (2), Voice Art na BET katika kipengele cha BET HER na kuandika rekodi kuwa binadamu mdogo zaidi kuwahi kushinda BET.

BET Her ni tuzo maalumu kwa nyimbo zinazotia moyo na kuwawezesha wanawake na kwa mara ya kwanza zilitolewa 2006 zikitambulika kama BET J Cool Like That hadi sasa Beyonce na Mary J Blige ndio wasanii walioshinda mara nyingi.

"Ninapomwambia Blue Ivy ninajivunia yeye ananiambia kuwa anajivunia mimi na kwamba ninafanya kazi nzuri. Ni tamu sana," Beyonce aliliambia Jarida la Vogue, Uingereza.

Jay Z ambaye ndiye msanii wa Hip Hop tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa Dola2.5 bilioni, katika mahojiano na The Sunday Times alizungumzia kuhusu malezi na kile alichojifunza kwa Blue Ivy.

"Unajua kuhisi kupendwa ndilo jambo muhimu zaidi ambalo mtoto anahitaji, sijali ikiwa mtoto wangu hataki kuwa katika muziki au michezo, lakini ilimradi anahisi kuungwa mkono na kupendwa, lolote linaweza kutokea," alisema Jay Z.

Blue Ivy amewahi kutumbuiza mara kadhaa, katika tuzo za Oscars 2022 akiwa na umri wa miaka 10 aliungana na mama yake Beyonce kutumbuiza wimbo wake 'Be Alive' uliyotumika katika filamu ya King Richard.

Mnamo Januari 2023 Blue Ivy aliungana tena na Beyonce kutumbuiza huko Dubai katika ufunguzi wa Hoteli ya Atlantis The Royal Resort ambapo walilipwa Dola24 milioni kwa shoo iliyochukua saa moja na nusu.

Sauti ya Blue Ivy ndio inasikika ikifanya simulizi katika kitabu cha watoto, Hair Love kilichoandikwa na Matthew A. Cherry ambaye amehusika katika filamu ya uhuishaji inayotokana na kitabu hicho iliyoshinda tuzo ya Oscar 2021.

Anatabiriwa anaweza kuja kufanya masuala ya mitindo na urembo na akiwa na miaka tisa, Februari 2021 alionyesha ni mwanamitindo mzuri baada ya kuungana na Beyonce kutangaza chapa mpya ya mavazi ya Adidas, Ivy Park.

Bibi yake Blue Ivy, Tina Knowles (Mama yake Beyonce) ambaye ni Mbunifu wa Mitindo alionyesha Instagram picha aliyopodolewa na mjukuu wake huyo na kumsifia ni mpambaji mzuri, anajua kucheza na makeup vilivyo.

Mdogo wake Blue Ivy, Rumi aliyezaliwa mwaka 2017 na pacha mwenzake Sir, amesikika katika albamu ya nane ya Beyonce, Cowboy Carter (2024) ambayo ilishinda tuzo mbili za Grammy ikiwa ni mara ya kwanza kwa Beyonce kushinda kipengele cha Albamu Bora.

Katika albamu hiyo iliyoshika namba moja chati ya Billboard 200 ikiwa ni ya nne mfululizo kwa Beyonce kufanya hivyo, Rumi ameungana na manguli wa Pop kama Paul McCartney na Stevie Wonder na kuna wale wa Country, Willie Nelson na Dolly Parton.