Lulu kama siyo sanaa angekuwa 'mama makusanya'

Muktasari:
- Kauli hii Lulu ameitoa alipoulizwa swali na Mwanaspoti kama anatarajia kupata mtoto wa tatu kwa mumewe Majizo, baada ya hivi karibuni kuposti picha kadhaa za ujauzito kwenye akaunti yake ya Instagram bila kuandika chochote kama ni picha za ujauzito wa zamani au wa sasa.
MWIGIZAJI wa Bongo Movie, Elizabeth Michael 'Lulu' amesema kama asingekuwa msanii angekuwa mama wa nyumbani mwenye watoto wengi.
Kauli hii Lulu ameitoa alipoulizwa swali na Mwanaspoti kama anatarajia kupata mtoto wa tatu kwa mumewe Majizo, baada ya hivi karibuni kuposti picha kadhaa za ujauzito kwenye akaunti yake ya Instagram bila kuandika chochote kama ni picha za ujauzito wa zamani au wa sasa.
"Naona watu wengi wameshtushwa na posti yangu ya ujauzito, sijajua shida iko wapi kama ni mjamzito kwa sasa, wapo waliosema mtoto wa pili bado mdogo na wengine kudai nazaa mfululizo na watoto hawapishani sana kiumri, ngoja niwaambie kitu kimoja leo Watanzania, mimi napenda sana watoto yaani kama nisingekuwa msanii ningeweza kuwa mama wa nyumbani mwenye watoto, yaani ningekuwa namuomba Mungu kila kukicha anipatie mtoto, kwangu ni faraja kubwa na wala sioni noma kuzaa mfululizo,” alisema Lulu ingawa hajaweka wazi kama ni picha za ujauzito wa zamani au anatarajia mtoto wa tatu na mume wake.
Lulu na mumewe Majizzo walifunga ndoa Februari 16, 2021 na mwaka huo huo walibarikiwa kupata mtoto wa kiume na baada ya mwaka na miezi mitano alipata mtoto wa pili wa kike.