Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

King Kikii wa ‘Kitambaa cheupe’ hatunae

King Pict
King Pict

Muktasari:

  • Taarifa za kifo cha King Kikii zimethibitishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa asubuhi ya leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Tanzania, Boniface Kikumbi maarufu King Kikii amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Novemba 15, 2024 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Taarifa za kifo cha King Kikii zimethibitishwa na mtoto wa marehemu Joseph Silumbe ameithibitishia Mwanaspoti kuwa Mwanamuziki huyo amefariki dunia.

“Ni kweli mzee hatunaye. Amefariki kama saa Saba usiku hivi. Kama familia huu ni msiba mzito kwetu lakini ni mipango ya Mungu hatuwezi kuizuia.

“Kuhusu taratibu za msiba, familia itazitoa,” amesema Joseph Silumbe

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa asubuhi ya leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

“Lala salama mzee wetu Boniface Kikumbi Mwanza Mpango (King Kikii), mwanamuziki mkongwe, jabali la rhumba na mtu mwenye utumishi uliotukuka katika tasnia ya muziki Tanzania.

“Tutauenzi mchango wako mkubwa katika muziki wa dansi Tanzania. Kwa miaka mingi umeburudisha, umefundisha, umeelimisha na uliipenda sana Tanzania,” ameandika Msigwa

Enzi za uhai wake, King Kikiii alitamba na vibao mbalimbali kikiwemo maarufu cha ‘Kitambaa cheupe’.


Endelea kufuatilia taarifa zaidi katika mitandao yetu ya kijamii