Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kajala anaingia Ibrah anatoka Konde Gang

KONDE Pict

Muktasari:

  • Ibraah na Kajala ni watu ambao kipindi cha mwisho, Kajala kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Harmonize, walikuwa wanaelewana sana na hata wawili hao walipoachana, Ibraah alinukuliwa akisema hakupendezwa na kitendo hicho.

HUKU madai ya kurudiana kwa Kajala na Harmonize yakishika kasi kila kona ya nchi, msanii Ibraah kutoka Lebo ya Konde Gang inayomilikiwa na Konde Boy imeelezwa anajiandaa kujiondoa chini ya staa huyo.

Ibraah na Kajala ni watu ambao kipindi cha mwisho, Kajala kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Harmonize, walikuwa wanaelewana sana na hata wawili hao walipoachana, Ibraah alinukuliwa akisema hakupendezwa na kitendo hicho.

Sasa ishu ya Ibraah kutaka kujindoa Konde Gang iko hivi. Usiku wa kuamkia leo Aprili 4, 2025 wakati video za Kajala na Harmonize za kuonyeshana mahaba zikitrend mitandaoni wakiwa kwenye sherehe ya bethidei ya mtoto wa Marioo na binti wa Kajala, Paula, muda huo huo Ibraah kupitia akaunti yake ya Instagram akaandika kuomba msaada wa mchango wa pesa za kujiondoa Konde Gang.

Ibraah ambaye mwaka 2020 alitambulishwa rasmi kuwa msanii wa lebo ya muziki ya Konde Gang, ameandika ujumbe kupitia ukurasa huo akiomba msaada kwa Watanzania wamchangie Sh1 bilioni ili aachane na Konde Gang.

"Daah hili mimi limenishinda narudi kwenu Watanzania mzee Konde anataka nimlipe Sh1 bilioni, mimi tangu nianze muziki sijawahi hata kuingiza hata robo ya Sh1 bilioni, kwa itakayempendeza hata ukiwa na jero, buku nisaidie wangu...mimi sitaki kupishana na Mzee Konde, ila hili suala la kulipia Sh1 bilioni linaninyima usingizi, hofu yangu pia kipaji changu kupotea na sina kazi nyingine. Kwa yeyote atakayejaaliwa chochote.

"Sio mbaya kukubali kuwa mimi ni kijana niliyetokea kwenye familia ya kimasikini na hili limenikuta sina budi kulileta kwenu maana pia ninachoamini nisingefika hapa bila ninyi mashabiki wangu na wadau mbalimbali katika sanaa na nje ya tasnia. Naomba msaada kwa yeyote anayeona anaweza kunisaidia."

Ibraah tangu alipotambulishwa katika Lebo hiyo ameachia nyimbo kali kadhaa ikiwamo; Dharau, Nitachelewa, Sawa, Wandoto, Jipinde, Rara na amefanya vizuri pia katika kolabo ambazo ameshirikishwa kama Mdomo ya Harmonize, Mateso ya Mabantu na nyimbo za singeli kama Do Let Me Go ya Kinata MC na Wivu ya JayCombat

Mwanaspoti lilimtafuta Ibraah ili kuthibitisha kile kilichosomeka katika akaunti yake naye alikiri ni kweli ameandika mwenyewe na wala sio mtu mwingine.

"Hapana akaunti ni yangu na mimi nimeandika na nipo siriaz kuomba msaada maana mimi sina hizo bilioni za kulipa, nimeamua kufanya uamuzi huu sababu bosi hataki kuwekeza, sasa mimi nitaishije, yeye anaangalia maisha yake tu," amesema Ibraah.

Aidha, Mwanaspoti lilimtafuta na Harmonize ambaye alisema hayuko tayari kujibu chochote.

"Sihitaji kujibu chochote kwenye hili," amesema Harmonize, ambaye juzi alionekana akiwa beneti na Kajala kuonyesha wawili hao wamerejesha penzi lao, ambalo limekuwa likifa na kufufuka mara kwa mara.