Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jux aendelea kuitikisa Nigeria, Ghana

JUX Pict

Muktasari:

  • Siku mbili zilizopita supastaa huyo aliachia Extended Playlist (EP) yenye ngoma saba ikiwamo ‘Si Mimi’, My Shayla, God Design, Celebration na nyinginezo.

MSANII Juma Jux ameendelea kushika namba moja kwenye chati mbalimbali za muziki nchini Nigeria na Ghana.

Siku mbili zilizopita supastaa huyo aliachia Extended Playlist (EP) yenye ngoma saba ikiwamo ‘Si Mimi’, My Shayla, God Design, Celebration na nyinginezo.

Jux alieleza kuwa EP hiyo ni maalumu kwa mkewe Priscilla Ajoke kama kumbukumbu kuelekea harusi yao itakayofanyika Jumatano hii jijini Dar es Salaam baada ya ile ya kifahari iliyotikisa Nigeria.

Ndani ya siku moja tangu kuachiwa kwa EP hiyo ‘A Day To Remember’ imefanya vizuri na kushika namba moja Nigeria kwenye ngoma zilizofanya vizuri.

Chati ya Nigeria iTunes imetoa Top 20 ya ngoma zilizofanya vizuri, God Design imeshika namba moja, ikafuata Si Mimi na namba tano Ololufemi aliyomshirikisha Diamond Platnumz. Wimbo wa singeli, Ex wa Nani aliomshirikisha Dvoice umekamata namba 16, 17 ni You, 18 Ololo, 19 My Shayla na 20 Celebration, hizi zote zikiwa kwenye EP yake mpya.

Mtandao wa Ghana iTunes umetaja albamu 10 zinazoongoza kusikilizwa na ya Jux ‘A Day To Remember’ ikiwa namba moja, na pia EP hiyo bado inaongoza Tanzania.

Baada ya mafanikio hayo Jux alisema; “Ninayo furaha kubwa kutangaza kwamba “A Day To Remember† inatamba kwenye iTunes, kwa nyimbo kadhaa kuingia kwenye chati na EP kufanikiwa kuingia kwenye Top 20 ya iTunes Nigeria ndani ya saa 24 tu,” aliandika na kuongeza;

“Hii ni hatua kubwa kwa muziki wa Afrika Mashariki, na nakuwa msanii wa kwanza kutoka kanda yetu kufikia mafanikio haya. Ahsanteni wote kwa upendo wenu, hakika hii ni Siku Ya Kukumbukwa.”

Ni kama ndoa ya Jux na mwigizaji huyo wa Nigeria imekuwa na neema kwenye karia yake ya muziki kwani hapo awali msanii huyo hakuwahi kushika kwenye chati za nchi za Afrika Magharibi zilizojaa nyota kibao wanaotamba Afrika na duniani.

Mbali na kuziteka nchi hizo lakini utakumbuka April 28 alishinda Tuzo ya Msanii Bora wa Afrika Mashariki kupitia tuzo za The Headies zilizotolewa usiku wa kuamkia Jijini Lagos akiwashinda Diamond Platnumz (Tanzania), Bien (Kenya), Bruce Melodie (Rwanda) na Azawi (Uganda).

Mwishoni mwa mwaka 2023 mastaa hao walidai kutoka pamoja kimapenzi, lakini haikuwekwa wazi hadi Agosti 2024 wakionekana kwenye sehemu mbalimbali za starehe Tanzania.

Hatimaye, Februari 7, 2025 wawili hao walithibitisha mapenzi yao kuwa ya kweli ambapo walifunga ndoa ya Kiislamu. Ikawa moja ya harusi kubwa zilizovuta hisia za mashabiki kutoka Tanzania, Nigeria, na kwingine.

Mbali na sherehe hiyo lakini pia walifanya shughuli nyingine iliyofanyika Nigeria ikiwa ni harusi ya Kitamaduni pamoja na kufunga ndoa ya kikristo huku wakisimamisha mitandao ya kijamii Afrika Mashariki.