Johari kwa sasa hataki shobo

Muktasari:
- Nyota huyo wa zamani wa Kaole Sanaa, ambaye kwa sasa ni Mtayarishaji na Mkurugenzi wa Lokoma TV, ameliambia Mwanaspoti, ameshakua kiakili hivyo hawezi kuanika uhusiano wake wa kimapenzi hadharani kama ilivyokuwa akifanya miaka ya nyuma kutokana na kujit-ambua na kuona haina maana kwa jamii.
MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu nchini, Blandina Chagula ‘Johari’, amesema kwa sasa hataki kabisa shobo za kuanika uhusiano wa kimapenzi mitandaoni kwani ametambua ni akili za kitoto.
Nyota huyo wa zamani wa Kaole Sanaa, ambaye kwa sasa ni Mtayarishaji na Mkurugenzi wa Lokoma TV, ameliambia Mwanaspoti, ameshakua kiakili hivyo hawezi kuanika uhusiano wake wa kimapenzi hadharani kama ilivyokuwa akifanya miaka ya nyuma kutokana na kujit-ambua na kuona haina maana kwa jamii.
“Unajua matukio huendana na wakati, unaponiuliza suala la uhusiano, ni kweli nipo katika malavidavi na mtu, ila kwa sasa akili yangu ime-kua na natambua lipi nikiweka wazi lina faida kwa jamii. Tabia ya kuanika uhusiano wa mapenzi mtandaoni ilikuwa ni akili ya utoto. Kwa sasa siwezi kufanya,” alisema.
Mwanadada huyo aliyewahi kuimba muziki wa kizazi kipya kupitia kundi la Crime Busters lililokuwa na wasanii kama Hussein Ramadhani ‘Swagger One’, Saleh Komba ‘Mourine’ na Renatus Pamba ‘Mr Simple’ alifafanua hata kutoonekana katika kumbi za starehe kama zamani, ina-sababishwa na staili ya maisha aliyochagua kutokana na kupitia changamoto nyingi za maisha.
Johari alisema, uamuzi wa kuepuka kujirusha hovyo inatokana na kutopenda kuonekana mtu wa hivyo na anapofanya mtoko basi huwa ni maalumu ili kuwafanya watu wamuone mpya.