Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jinsi ya kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume bila kutumia dawa

 MAMBO vipi wapenzi wasomaji wa gazeti la mwanaspoti katika kona ya MAPENZI, leo nimeona nirudi na kuanza kutoa somo kuhusu janga hili la dunia kwa wanaume wengi.

Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolo-jia walizonazo wanaume.Lakini kwa kufupisha mlo-longo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua wa-naume wengi duniani.

Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni kukosa msisimko, kushindwa kurudia tendo na kukosa kabisa nguvu, huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia kama pacha wa janga hili ambalo linawasumbua zaidi wanaume, in-gawa na wanawake wanakabiliwa na sehemu ndogo ya tatizo hili.Hata hivyo, uchunguzi wa hivi karibuni uliowahusisha wanaume wanaofika kliniki au kupata tiba za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume umeonesha sio wanaume wengi wenye sababu za kibaiolo-jia zinazowafanya wakose nguvu za kiume, isipokuwa wengi wao huwa na matatizo ya kisaikolojia zaidi ambayo wahusika wanaweza kujiponya nayo bila hata kutu-mia vidonge wala dawa za miti shamba.

Ingawa matabibu wana-taja magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya zinaa, unene wa kupita kiasi, umri mkubwa kuwa ndiyo chanzo cha wanaume kupungukiwa na nguvu za kiume, lakini imebainika kuwa idadi kubwa ya wanaume wanaofi-ka hospitalini kutafuta nguvu za kiume hawana magonjwa hayo.Huu ni ushahidi wanaokabili-wa na janga hili wamebeba tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kimawazo zaidi kuliko hali halisi.

Ukweli wa mambo ulioibuliwa na wanasaikolojia umebaini wale wote wanaolalamikia/lalamikiwa kuwa hawana nguvu iwe ya kufika kileleni mapema, kutokuwa na msisimko na kushindwa kurudia tendo wamekosa maarifa tu ya kufahamu na hawaijui miili yao na wanaishi kwa kusikia zaidi ya kujitambua.Katika hali ya kawaida kila mwanadamu ameumbwa kwa jinsi yake na inapotokea kushabihiana basi ni bahati.

Mara nyingi usawa hupatikana kwa mmoja kujifunza au kusaidiwa kufikia kiwango cha mtu anayemhitaji kuwa nae katika maisha hasa ya kimapenzi.Jambo hili wataalamu wanase-ma miili iko tayari kutii mafunzo na kubadilisha tabia zake kulin-gana na utashi wa mhusika.

 

HOFU

Tatizo kubwa lililopo kwa wapenzi wengi wanaolalamikia upungufu wa nguvu, maisha yao wanayachezea kwenye viwanja vya wenzao wanaokutana nao katika vijiwe na sehemu za kazi.

Usikivu wa mazungumzo kuto-ka kwa wanaume wengine wenye uwezo wa kwenda mara nne hadi saba katika tendo au wanatumia dakika arobaini kufika kileleni umewafanya wanaume wengi kujihisi tu kuwa wao wana kasoro eti kwa kuwa huishia mara mbili au moja katika kufanya tendo.Dhana ya kujiona ni mwenye kasoro inapojengeka akilini mwa mwanamume, huchipua hofu na hatimaye kumfanya ashindwe kabisa kusisimka anapofikiria au kukutana na mwanamke. Matokeo ya hangaiko la akili hushusha uwezo wa mwili na kumwongoza mtu kwenye kuwaza ugonjwa kisha kukimbilia hospitali au kwa waganga kutafuta tiba ya ugonjwa ambao kimsingi hanao.

Hata hivyo, ukweli uko wazi kukimbilia kutafuta uwezo wa kufanya mapenzi mara sita au saba hakumfanyi mwanamume awe mlinganifu mwenye kusifiwa na wanawake wengi, kwani si wanawake wote wana uwezo wa kufanya mapenzi kwa raundi hizo na si wote wanapenda kutumia dakika 30 kimahaba.

Wapo wa-naokinai mapema na huona kero kuwa na wanaume ving’ang’anizi wenye sifa za kuwaganda.Kwa kufahamu haya utagun-dua kukimbilia kutafuta tiba ya kumudu kwenda mara saba ni jitihada mfu kabisa zisizohitajika katika maisha ya mwanamume hasa ukizingatia wenye uwezo wa kufanya mapenzi mara nyingi hawakuzaliwa hivyo, bali waliji-zoeza kupitia mazingira ya malezi na makuzi yao. Maana hawezi kuwa mzoefu wa raundi mvulana aliyelelewa katika mafundisho ya kukatazwa ngono na kulindwa hadi akakua.

Kadhalika hawezi kuwa hodari wa kimapenzi msichana aliye-fundishwa kujitunza, yote yatakay-ofuata kwa mvulana au msichana kutokea baada ya kupandwa na tabia chipukizi za ukubwani. Kwa msingi huo mwanamume ana jukumu la kuutengeneza mwili wake uwe katika staili aitakayo. Ndiyo maana kuna wengine hawa-mudu kulala bila kufanya ngono, hii ikiwa na maana kuwa wameji-zoeza tu, si kwamba wameumbwa na nguvu hizo.

 

Itaendelea Wiki ijayo. Kwa mawasiliano, nipigie 0712313191, barua pepe, zubagy@yahoo.com au zubagyakilimia@gmail.com. SOMA KITABU CHANGU CHA KISS, HUG AND LOVE; kin-auzwa Tsh 4000/= tu.