Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JB apangua tuhuma za kutoka kimapenzi na wasanii wenzake

JB Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa zamani aliyeanza kutamba na michezo ya katika runinga miaka ya 1990, amekuwa akielezwa kuwa na tabia ya kuwa na uhusiano na baadhi ya wasanii wa kike wanaoshiriki kazi anazoziandaa, lakini amesema ukweli sivyo ulivyo.

MWIGIZAJI mkongwe na mtayarishaji wa filamu nchini, Jacob Stephen ‘JB’ amekanusha madai kwamba amekuwa akitumia nafasi yake kutoka kimapenzi na wasanii anaofanya nao kazi, akisema wanaomzushia hivyo hawajui alivyo.

Nyota huyo wa zamani aliyeanza kutamba na michezo ya katika runinga miaka ya 1990, amekuwa akielezwa kuwa na tabia ya kuwa na uhusiano na baadhi ya wasanii wa kike wanaoshiriki kazi anazoziandaa, lakini amesema ukweli sivyo ulivyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, JB alisema hizo habari ni za uzushi na kwamba kuwa karibu na wasanii wengi wa kike wa filamu inatokana na  kupenda kuwapa moyo wa kufanya kazi zaidi, lakini mara nyingi amekuwa akiwapa maua hadharani wale wote wanaofanya vizuri.

“Hayo mambo ni ya kizamani sana, mtu kama mimi mwenye heshima katika hii tasnia nawezaje kufanya huo upuuzi? Unajua wenye tasnia ya filamu tunao waigizaji bora wa kike, sasa tukiwa tunaleta tamaa ya kimwili hatutawasaidia hawa wasanii, lakini siri yangu kubwa ya kuwa karibu na waigizaji wa kike ni kuwapa moyo na wengine huwa nawapa maua yao wakiwa hai kwa ufanisi wao, nafanya hivyo kwa vile sitaki kusubiri mtu afe ndipo nimsifie kinafiki.

“Nafanya hivi kwa sababu wapo watu wachache tu wenye kutambua thamani ya utu wa wasanii wa kike.”