Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Lulu Juakali yaibua mastaa

Muktasari:

  • Lulu amechukua nafasi ya Maria ambaye alikuwa anacheza kipengele cha mfanyakazi wa kampuni na anawagonganisha mabosi zake kwenye mahusiano ambao ni Madevu na Frank.

KUBADILISHWA kwa Maria kwenye Tamthilia ya Juakali na nafasi yake kuchukuliwa na Elizabeth Michael 'Lulu' kumewaibua watayarishaji wakimkingia kifua mtayarishaji na muongozaji wa tamthilia hiyo, Leah Richard 'Mwendamseke 'Lamata'.

Lulu amechukua nafasi ya Maria ambaye alikuwa anacheza kipengele cha mfanyakazi wa kampuni na anawagonganisha mabosi zake kwenye mahusiano ambao ni Madevu na Frank.

Siku chache baada ya kuonekana kwenye vipande vya tamthilia hiyo na mashabiki kumjia juu Lamata, mwandaaji huyo amekosea kuwabadilishia, huku nyuma ametetewa.

Mtayarishaji na mwigizaji, Chuchu Hans amesema ni mapema sana mashabiki kumchukia Lulu kwani ndio kwanza ameanza, huku akiweka wazi Lamata hana kosa kufanya hivyo.

"Kubadilishwa kwa msanii haijaanza leo wala jana na inatokea kwa sababu maalumu. Huwezi kukatisha stori kutokana na kukosekana kwa mtu mmoja, amefanya hivyo kwa sababu maalumu na huwa inatokea," amesema.

Msanii Zuwena Mohammed 'Shilole' amesema anamfahamu vizuri Lulu na watu wasubiri awaonyeshe ufundi wake na nafasi aliyopewa anaweza kuifanya kwa usahihi.

"Wampe muda kwanza halafu waone kama atashindwa kufanya alichokuwa anakifanya aliyepita. Tamthilia bado inaendelea, waendelee kuifuatilia, watamuelewa tu," amesema.