Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Instagram yamweka njia panda Jenifer Kanumba

Muktasari:

  • Jenifer na msanii mwenzake Othumani Njaidi ’Patrick’, ni kati ya wasanii walioibuliwa na marehemu Steven Kanumba katika filamu ya ‘This is It’ na ‘Uncle JJ’ zilizofanya vizuri sokoni.

Dar es Salaam. Mcheza filamu Hanifa Daudi ‘Jenifer’ ameingia matatani shuleni anaposoma baada ya kuwepo kwa mtu anayetumia jina lake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.


Jenifer na msanii mwenzake Othumani Njaidi ’Patrick’, ni kati ya wasanii walioibuliwa na marehemu Steven Kanumba katika filamu ya ‘This is It’ na ‘Uncle JJ’ zilizofanya vizuri sokoni.


Tayari sasa wameshakuwa wakubwa na mwaka huu Jenifer atafikisha miaka 18, akiwa kidato cha tano katika shule ya Sekondari St. Christina iliyopo Jijini Tanga.


Mama wa Jenifer, Rose Mogela amesema safari hii mtoto wake alipofunga shule kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu ya Pasaka, amemuambia kuwa alisimamishwa mbele ya wanafunzi wenzake na kukanywa na walimu kuhusu suala hilo la kumiliki Instagram wakati siyo kweli hana kitu kama hicho.


Kutokana na hilo Rose ameomba anayemiliki kurasa huo na kutumia jina la mtoto wake kuacha mara moja na kuongeza kuwa yupo katika mpango wa kwenda kuripoti jambo hilo Polisi.
Mkuu wa shule Sekondari St. Christina anayosoma Jenifer aliyejitambulisha kwa jina  la Mwalimu Kaniki amekiri kumkanya Jenifer na suala hilo na kuongeza kuwa wazazi wanapokuwa na watoto wa aina ya Jenifer ambao ni maarufu wanapaswa kuwa waangalifu katika malezi.


“Ni kweli Jenifer tumempokea hapa shuleni tayari akiwa maarufu, lakini tumemuandikisha kama wanafunzi wengine na anapaswa kufuata sheria na taratibu zote zilizowekwa kama ambavyo zipo kwenye fomu wanayotakiwa kujaza kabla ya kuanza shule na pamoja kukana kutotumia mtandao huo sisi bado tunafuatilia kubaini ukweli,” alisema Kaniki.


Hata hivyo ameeleza kuwa bado wataendelea kumshauri namna ya  kuishi shuleni hapo ili asijikute anaingia katika mikono mibaya kwa kuwa lengo lao ni  kumsaidia kufikia  ndoto zake.