Huyu ndiye Fid Q au Mzee Mbuzi

Muktasari:
- Ni miaka zaidi ya 20 yupo katika muziki akitoa ngoma kali za Hip Hop huku akishiriki kuinua wasanii wengi wa muziki huo kupitia kolabo na miradi yake mingine kama Fidstyle Friday Show. Huyu ndiye Fid Q au Mzee Mbuzi
Kwa mujibu wa Fid Q, uwezo wake wa kuandika mashairi unatokana na tabia aliyojijengea ya kujisomea vitabu kitu ambacho kimemjenga na ndilo chimbuko la albamu yake ya tatu, KitaaOlojia iliyotoka Agosti 2019 ikiwa na nyimbo 23.
Ni miaka zaidi ya 20 yupo katika muziki akitoa ngoma kali za Hip Hop huku akishiriki kuinua wasanii wengi wa muziki huo kupitia kolabo na miradi yake mingine kama Fidstyle Friday Show. Huyu ndiye Fid Q au Mzee Mbuzi
1. Hardmad ndiye mtu wa kwanza kumpeleka Fid Q pale MJ Records kwa Master Jay aliporekodi wimbo wake 'Huyu na Yule' akimshirikisha Mr. Paul, wimbo huo ulimtambulisha vizuri ndani ya Bongo Fleva.

Baadaye akarekodi ngoma nyingine, 'Fid Q Dot Com' ndani ya Baucha Records ukiwa ndio wimbo wa kwanza kurekodi katika studio hiyo, vilevile huu ni wimbo wa kwanza kwa Rapa huyo kuufanyia video.
2. Albamu ya kwanza ya Fid Q, Vina Mwanzo Kati na Mwisho (2005) chini ya Bongo Records, ni msanii mmoja tu wa kike aliyeshirikishwa ambaye ni Lady Jaydee aliyesikika katika wimbo, Kadi na Ua Rose.
3. Kwa jumla tayari Fid Q ametoa albamu tatu, Vina Mwanzo Kati na Mwisho (2005), Propaganda (2009), KitaaOLOJIA (2019) na Neno (2024) ambayo kashirikiana na Lord Eyes, rapa kutoka makundi ya Nako 2 Nako Soldiers na Weusi.
4. Tuzo ya kwanza Fid Q kushinda katika Tanzania Music Awards (TMA) ilikuwaa 2006 kupitia wimbo wake, Mwanza (2005) ulioshinda kama Wimbo Bora wa Hip Hop na kwa jumla ameshinda tuzo nne za TMA akifanya hivyo kwa mara mwisho 2014.

5. Fid Q ana rekodi lebo yake, Cheusi Dawa Entertainment, unaungana na wakali wengine wa Rap wa kitambo ambao wana lebo zao kama AY (Unity Entertainment), Dark Master ana rekodi lebo yake, A.B.C (Another Bad Creation/Chemba) n.k.
Utakumbuka AY kupitia Unity Entertainment aliwahi kuwasaini Ommy Dimpoz na Stereo, huku Fid Q kupitia Cheusi Dawa Entertainment akimsaini Big Jahman ambaye ameshirikiana kwenye nyimbo kama Mabundi, Bambam na Umenituliza.
6. Tuzo ya kwanza ya kimataifa kwa Witness, mwanachama wa zamani kundi la Wakilisha kushinda katika muziki inatokea Channel O baada ya kufanya vizuri na wimbo wake, Zero (2008) uliotayarishwa na Prodyuza Eryne na kumshirikisha Fid Q.
Ikumbukwe Witness ni miongoni mwa wanawake waliofanya vizuri katika muziki wa Hip Hop, alikuwa mshindi wa Coca-Cola Popstar 2004 na kuunda kundi la Wakilisha na wezake wawili ambao ni Langa na Shaa.
7. Hadi sasa Fid Q ndiye msanii wa Hip Hop Bongo ambaye Rosa Ree kashirikiana naye katika nyimbo nyingi zaidi, wawili hao tayari wametoa nyimbo nne ambazo ni Ole Chizza (2018), Korasi (2019), Trust (2022) na Bigman (2023).

8. Kwa mujibu wa Stamina kupitia wimbo wake, Mr. Boniventure (2021) aliomshirikisha Mr. T Touch, ukimtoa Fid Q na Roma hakuna Rapa Bongo anayemtisha kwa uandishi na michano.
Utakumbuka Stamina alishafanya kolabo kadhaa na Fid Q kama Wazo la Leo (2013), Like Father Like Son (2015) n.k, pia amefanya refix ya wimbo wa Fid Q, Mwanza (2005) kisha kuja na wake unaojulikana kama Moro Moro (2015).
9. Kundi la Wakali Kwanza linaloundwa na Joslin, Makamua na Q Jay ndio walitakiwa kusikika katika wimbo wa Fid Q, Usinikubali Haraka (2009), ila Matonya alipousikika akaupenda wimbo huo na kurekodi na mengine sasa ni historia.
10. Fid Q ni miongoni mwa wasanii wanaotumia majina ya wanyanya, yeye anajiita, Mzee Mbuzi, anajiita Mbuzi yaani 'G.O.A.T' kwa lugha ya Kiingerza akimaanisha the Greatest of All Time (Bora wa Muda Wote) akiwa na miaka 20 katika muziki.
Wasanii wengine wanaotumia majina ya wasanii kwa sababu mbalimbali ni Mr. Blue (Nyani Mzee), Diamond Platnumz (Simba), Harmonize (Tembo), Rayvanny (Chui), Country Boy (Fisi), Dudu Baya (Mamba), Afande Sele (Simba Dume) n.k.
WIKI IJAYO > Msanii anayefuata ni Lamar.