Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huu sasa mtihani kwa Paula!

DIAMOND Pict

Muktasari:

  • Staa huyo wa ngoma ya Nitafanyaje, aliyoipiga katika miondoko ya singeli, amesaini mkataba mpya wa kampuni ya SBC Tanzania Ltd baada ya ule wa awali kufikia tamati.

SUPASTAA wa Next Level Music (NLM), Rayvanny amedondosha ngoma yake, Pere (2025), akishirikiana na Marioo na Harmonize. Kolabo hii kwa namna moja au nyingine ni mtihani kwa Paula, binti wa Kajala Masanja na P-Funk Majani.

Inaweza kuwa mtihani kwa Paula kwa sababu ya historia isiyoweza kufutika kati yake na Rayvanny, Harmonize na Marioo ambaye ni mpenzi na mzazi mwenzake wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja, Amarah, aliyezaliwa Mei 2024.

Ngoma hiyo iliyotayarishwa na S2kizzy, mkurugenzi wa Pluto Republic Studios tangu ilipotoka imejadiliwa sana kutokana na ukubwa wa wasanii hao, lakini kubwa zaidi jinsi ambavyo kazi walizowahi kufanya awali zilivyoacha alama.

Mathalan kwa Marioo na Harmonize, Pere (2025) ni kolabo ya tano kwao baada ya awali kuachia Naogopa (2022), Away (2024), Disconnect (2024) na Wangu (2024) kutoka katika albamu ya pili ya Marioo. Ila kwa Paula, kwake Pere ni zaidi ya wimbo, unasikika tofauti na unachezeka kwa mtindo ambao ni tofauti na wengi wanavyoweza kucheza, hivyo huenda akapata tabu kufurahia ngoma hiyo mbele ya umma kama alivyofanya kwa nyingine za Marioo.

Sababu ni kwamba, Rayvanny ambaye ndiye hasa mmiliki wa wimbo huo ni mpenzi wake wa zamani ambaye hawakuachana kwa amani kwani kila mmoja alimtuhumu mwenzake kwa ubaya uliomtia aibu isiyoelezeka.

"Najuta hata kukufahamu maana wewe ndio umesababisha dunia nzima inione mimi ni mtu mbaya, bora hata ningekaa na usichana wangu," aliwahi kusema Paula katika reality show yake, Behind The Gram.

"Ulisababisha nitukanwe na dunia nzima kisa upuuzi wako. Mpaka leo hii wewe ndio unanipa kazi ya kuwaonyesha watu mimi siko hivyo wanavyofikiria," alisema Paula katika shoo hiyo iliyoruka Mei 2023.

Naye Rayvanny alijibu mashambulizi akidai Paula alimsaliti kwa kutembea na kaka yake katika muziki, na hilo likaacha maswali ni nani huyo? Ikumbukwe Rayvanny amelelewa zaidi kimuziki na Madee na Diamond Platnumz. Je ni mmoja kati yao au kuna mwingine?

Walipoachana, Rayvanny akarejea kwa mpenzi na mama mtoto wake Fahyma, huku Paula akizama katika uhusiano mpya na Marioo, mwanamuziki aliyetoka na kibao chake, Dar Kugumu (2018) na hadi leo hapoi wala haboi.

Mwezi mmoja baada ya Rayvanny na Paula kuraruana mtandaoni, Kajala alizungumza akimuelezea mwanawe kuwa ana msongo wa mawazo na hiyo isiwe sababu ya kuruhusu kutumiwa kama alivyofanya Rayvanny, hivyo awe makini na Marioo.

"Mtu anajua kama una stresi zako anakutumia, amepita huyu Rayvanny amekutumia halafu nini? Anakuchoresha tu bila sababu usimpe hiyo nafasi Marioo akutumie," alisema Kajala, staa wa filamu, Kijiji cha Tambua Haki (2012).

Ikumbukwe Rayvanny aliingia katika maisha ya Paula kipindi ambacho Kajala ana uhusiano na Harmonize na kuanzia hapa mambo yalianza kuvurugika maana haikuchukua muda picha za Harmonize zilisambaa mtandaoni ikidaiwa alikuwa anamtaka Paula.

Hiyo ilisababisha Harmonize kuwapeleka polisi Kajala, Paula na Rayvanny akiwatuhumu kumchafua na kabla kufikia hapa, Rayvanny na Harmonize walikuwa hawaelewani, hivyo ilionekana sio jambo la kumchafua tu, bali la kumshusha kimuziki.

Akizungumza na wanahabari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Novemba 2021, Harmonize alidai  inafikia hatua inaogofya kuingia katika uhusiano na wanawake wa Bongo maana anaona wanatumiwa na mahasimu kummaliza.

Wakati huo mgogoro kati ya Harmonize na WCB Wasafi ulikuwa bado na ufukuta, hivyo kitendo cha Rayvanny aliyekuwa katika lebo hiyo kwenda kuwa na Paula baada ya kuona Harmonize yupo na Kajala kilitafsiriwa kama penzi lenye ajenda nyingine nyuma yake.

Kwa ujumla mgogoro kati ya Rayvanny, Harmonize na Kajala uliacha majeraha ya kihisia kwa Paula. Kwa hiyo wimbo 'Pere' unaweza usiwe muziki mzuri kwake hata kama mpenzi wake Marioo kashirikishwa. Mei 2023, Kajala kupitia Behind The Gram alisisika akisema Paula aliwahi kumueleza kuwa madai ya kuambiwa ametoka na mwanaume wa mama yake yalimuumiza sana hasa baada ya rafiki zake kumhusisha na Harmonize.

"Paula anaweza kuwa amesema nimekusamehe kwa sababu mimi ni mama yake, ananipenda lakini sijui moyo uko vipi," alisema Kajala na kuongeza:

"Kuna siku alishawahi kunitamkia akaniambia ‘unadhani mimi watoto wenzangu wananichukulia vipi kwamba mimi nime-share mwanaume na mama yangu?' akaendelea kusema hii itanila maisha yangu yote.”

Ingawa kwa sasa hali imetulia, bado ni vigumu kuamini kuna siku unaweza kumuona Paula TikTok au Snapchat akiwa amejirekodi akiimba wimbo huo (Pere) kwa furaha, labda kipande alichoimba Marioo ila kile cha Rayvanny na Harmonize ni mtihani kwake.