Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hivi ndivyo maprodyuza wanavyofaidisha wasanii

KISHAKAJI Pict

Muktasari:

  • Kweli, prodyuza anafikiwa anakutana na msanii mkubwa na msanii anakubali midundo yake. Wanatengeneza goma la kwanza linaenda mjini

MAPRODYUZA wa muziki Tanzania ni miongoni mwa makundi yanayoongoza kulia njaa. Wakiumwa mbio kwenye mitandao ya kijamii kuomba msaada.

Wakipatwa matatizo nduki kwenye Instagram kuomba wadau wawachangie. Na mara zote wanapoomba misaada hii wadau huwauliza swali moja “kwani hizi kazi mnazofanya na zinahiti mnafanyaga kama sadaka, hamlipwi?”

JIBU ni NDIYO… hawalipwi wanavyostahili na leo nitakupa mchezo mzima ulivyo.

Picha huanza pale prodyuza anapojitafuta; anatengeneza midundo mikali lakini shida ni kwamba maprodyuza wanaamini ili kutoboa ni lazima biti zake zitumiwe na wasanii wakubwa. Ukigonga biti kali halafu ikampata Zuchu, Nandy, Mondi, Jux hapo unaingia mjini moja kwa moja. Haina mbambamba. Kwa hiyo unakuta prodyuza anafanya juu chini kuupata ukaribu wa msanii mkubwa ili ampatie biti zake.

Kweli, prodyuza anafikiwa anakutana na msanii mkubwa na msanii anakubali midundo yake. Wanatengeneza goma la kwanza linaenda mjini.

KISH 01

Msanii anaona dogo mkali anarudi tena kwake watengeneze ngoma zingine nyingi. Sasa kwa sababu ile ya kwanza walitengeneza bure hizi nyingine msanii anakuwa anampoza dogo laki laki, buku hamsini hamsini.

Vile anavyojisikia. Kuna taimu hawa maprodyuza wanaotajwa kwenye ngoma kubwa wanalipwa mpaka buku teni teni za nauli tu.

Unakuta prodyuza anaumizwa na malipo hayo ya kinyonyaji ambayo kwanza hayalingani na hadhi ya kazi anayoifanya, lakini pia ni malipo yenye ukomo yaani unapewa buku teni studio nd'o mmemalizana. Msanii anakwenda kutengeneza mamilioni na hiyo ngoma lakini prodyuza hana haki hata mara moja.

Prodyuza anatamani kufunguka ya moyoni kwa msanii mkubwa lakini sasa akiwaza vipi nikisema halafu msanii mkubwa akimaindi akagoma kunipa kazi.

Akaacha kunialika kwenye hausi pati zake. Akaacha kuongozana na mimi kwenye maiventi itakuwaje? Unakuta prodyuza anaamua kukukubali kuendelea kuteseka.

Mwisho wa siku nd'o hivyo kila hit song unasikia jina la prodyuza linatajwa. Mtaani mashabiki mnajua prodyuza atakuwa anavuta mtonyo kama wote kumbe hamna kitu, njaa mbaya.

KISH 02

Natamani niseme tatizo wanalau maprodyuza kwa kukubali kufanya kazi bila maelewano ya jinsi gani watapata stahiki zao, lakini nafsi yangu inakataa.

Nafsi yangu inanimbia tatizo wanalo wasanii wakubwa kwa sababu wanajua maprodyuza wadogo bado ni washamba na kutrendi. Bado ni washamba wa kuwa karibu na wasanii wakubwa. Bado wanajitafuta. Bado wanapambania namna ya kutengeneza na kukuza majina.

Kwa hiyo wasanii wakubwa wanaamua kutumia upenyo huo kuwanyonya.

Baadhi ya maprodyuza walijariabu kuweka mguu chini na kupambania haki zao, lakini mwisho wa siku wakaishia kukimbiwa na wasanii wakubwa na tangu hapo usanii wao ukawa kama umefifia hivi. Kwenye hili wasanii wakubwa wanatakiwa kubadilika.