Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hamisa: Ndoa na Aziz KI sio fasheni

HAMISA Pict

Muktasari:

  • Hivi karibuni kumezuka maneno maneno mitandaoni ya kusema ndoa ya Hamisa Mobetto na Aziz KI itaweza kuvunjika muda sio mrefu kutoka na Aziz KI kuondoka Tanzania.

MWANAMITINDO na mjasiriamali maarufu wa Tanzania, Hamisa Mobetto, amefunguka kuwa, watu wasimfikirie ameamua kuingia katika ndoa kama maonyesho, bali amedhamiria kwenda kuwa mke anayestahili kuwa mfano wa kuigwa na hatarajii kutoka kwenye ndoa ng’o.

Akizungumza na Mwanaspoti, Hamisa ambaye hivi karibuni amekuwa gumzo kila kona baada ya Aziz KI kuachana na Yanga kwenda kuitumikia klabu ya Wydad Athletic ya Morocco alisema, anajua wazi watu wengi wanamuhesabia siku kama ilivyo kwa mastaa wengine, lakini atawashangaza walimwengu wenye kusubiri ndoa za watu kuvunjika.

“Najua wazi watu watakuwa wananihesabia siku ndani ya ndoa yangu, lakini ukweli ni kwamba nitawashangaza watu wengi sana na sina sababu ya kuacha kuwa mke bora na mwenye heshima kwa mume wangu watanihesabia hadi watachoka wenyewe maana mimi nakomaa,” alisema Hamisa Mobetto.

Hivi karibuni kumezuka maneno maneno mitandaoni ya kusema ndoa ya Hamisa Mobetto na Aziz KI itaweza kuvunjika muda sio mrefu kutoka na Aziz KI kuondoka Tanzania.