Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gozbert: Walitaka kuniua, afunguka mazito sababu kuchoma gari

Muktasari:

  • Goodluck amefunguka hayo na mengine mengi kupitia ukurasa wake wa Youtube, amesema gari ameichoma moto kwa sababu moja, Mungu anayemtumikia ana wivu sana hataki utukufu wake uchukuliwe na mtu wa aina yeyote.

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Goodluck Gozbert amesema kuchoma gari lake moto asihusishwe nabii yeyote, kwani wapo waliokuwa wanataka kumuua ili kesi iende kwa nabii huyo.

Goodluck amefunguka hayo na mengine mengi kupitia ukurasa wake wa Youtube, amesema gari ameichoma moto kwa sababu moja, Mungu anayemtumikia ana wivu sana hataki utukufu wake uchukuliwe na mtu wa aina yeyote.

"Mimi Mungu aliniambia nisiendeshe lile gari wala kumpa mtu kuendesha, na Mungu akikuelekeza kitu haihitaji kujieleza kwanini anakwambia hivyo, na  ninapozungumza hapa najua kuna wale manabii wa facebook, kuna wale watumishi wa youtube kuna wale watu wa kukata vipande hiki kimesemwa hivi aliambiwa hivi tulisema hivi, niwaambie tu kitu ambacho mtu hujakipitia huwezi kuamini. Mimi nilikuwa nasumbuana sana na Mungu, nilikuwa nikienda kuiwasha gari tu hata kama siiendeshi basi Mungu ananielekeza kuwa injini itapasuka, lakini bado nilikuwa napingana naye na naendelea kuliendesha gari huku namuomba Mungu huyo huyo," amesema mwimbaji huyo na kuongeza;

"Baada ya kuambiwa hivyo,  ikaanza kutokea vipindi vya misiba mara tatu, ilianza  kutangazika nimefariki, msiba mara ya  kwanza ilikuwa Mungu kunificha kunihifadhi, kuniondoa kwenye rada, kunitoa eneo ambalo nitaacha kuhangaika, yaani ilikuwa kipindi cha wanaonidai walikuwa hawanidai na  ninao wadai walikuwa hawanilipi, nikafanya majaribio naweka nyimbo zangu Youtube usiku nazikuta asubuhi ziko vilevile, na kipindi hicho nilikuwa kwenye maono, ndoto za hapa na pale  mbaya zilikuwa nyingi sana, nilikuwa naota nipo  makaburini. Natembea kwenye makaburi yote yaliyonizunguka, nikawa naendelea kufanya maombi, mara naona mbwa wamenizunguka, sasa katika ulimwengu wa kiroho mambo ya kiroho  ukiongea hivi watu wanajua ni  utani," amesema Goodluck bila ya kumtaja nabii gani asihusishwe.

Goodluck aliendelea kusema, hapo ndio Mungu alimwambia ndio sababu ya kukwambia aache  kuendesha lile gari, kwani kuna watu walitaka kumuua.

"Nilipotokewa na hivyo vitu, Mungu  alikuja kuniambia hiyo ndio sababu ya  kukukataza usiendeshe gari lako, sababu kuna watu walitaka kukuua na walijaribu kwa njia nyingine zozote wakashindwa, na  wala sio nabii mkuu naomba hapa nieleweke vizuri, Mungu alisema, watu waliokuwa wanataka kuniua ni moja nikiwa naendesha hilo gari wangenimaliza halafu kesi ingeenda kwa aliyenipa gari, nikamuuliza Mungu nani alitaka kuniua? hakuniambia, mimi nikaendelea na mambo yangu.

"Sasa kuna watu wanashikilia na kuniandama kwa kuniambia kuwa mimi nimeibiwa nyota, ndio maana  sisikiki kwenye kuimba, ila  hawajui nani aliyetaka kuniua wao wanapiga tu kelele za mimi nitoe nyimbo, hawajui napitia masaibu gani, kumbe nilikuwa nahangaikia uhai wangu, nikaja kuzushiwa kifo tena. Kama mnakumbuka nikajirekodi katika mtandao wa Tiktok kuwa  mimi siwezi kufa kama wanavyodhani watu, japo watu  walisema sana kuwa nataka kutoa wimbo, ila haikuwa hivyo na  siwezi kufa sababu ya watu hao walishashindwa, na  siku nikifa Rais  atakayekuwa ndiye atakayetangaza kifo changu, na Mungu asije akaniinua akaja mtu mwingine akasema mimi ndio niliyetabiri nitainuka, au akasema sababu wamenipa nguvu za giza ndio nikainuka, Mungu anataka utukufu wake mwenyewe, ndiye aliyeniinua na kunipa uzima, ndiye aliyeniambia acha  kuendesha gari , tena kuna wakati Mungu aliniambia nigawe viatu vyangu,  nguo zangu kwa wenye uhitaji  na yote haya. Mimi huwa siongeagi ila Mungu amenipa kibali cha kuongea leo , sababu kuna taarifa nyingi sana za uongo zinasambaa sana" alisema Goodluck

Mbali na hayo Goodluck aliendelea kusema, kuna kipindi Mungu alimpitisha akawa ana hamu ya kufunga na kuomba tu, alikuwa anaweza kufunga siku saba au tano hadi tatu.

 "Hiki ni kitu cha kawaida, na naweza kumaliza mfungo huu na nikaunganisha mfungo mwingine, watu wananiambia nimekonda, lakini hapa nilipo mimi siumwi, sina tatizo la kiafya, ila kuna kitu cha kiroho kilinitokea katika maisha yangu kilinisukuma kuwa hivyo, na naamini labda sasa naweza kuishi kama watu wengine wanavyoishi.

"Na sababu ya kuwa kimya, haihusiani na menejimenti yangu kama baadhi ya watu wanavyosema , ila tangu mwaka 2017 nilikiwa natamani kuwa kile ninachokifanya nataka kujua itakuwaje, yaani mwaka 2017 nafikiria 2020 inakuwaje ,2020 nafikiria 2025 inakuwaje, nimejitengenezea mazingira ya kujitafakari na mkataba wangu uliisha katika menejimenti yangu toka 2017 , tukirudi nyuma mwaka 2021 hadi 2024 tunaweza kujadili kwanini nilikuwa kimya. Nilikuwa kimya kuna vitu vilisababisha kuwa hivyo.

"Tangu mwaka 2017 tayari nilianza kufikiria na kutafakari namna gani ambayo muziki wetu wa injili unaweza kuwa kama wakati nakuwa, yaani wakati niko mdogo ulikuwa unasikia nyimbo hizi, miaka yetu ilikuwa unachukua uwanja unajaza asilimia ya watu wengi wanaimba nyimbo za injili, ikafikia hatua hilo suala hakuna tena, sasa ukiona vitu kama hivyo vinapotea lazima uwaze kama muimbaji.

Siku mbili zilizopita kuna video iliyosambaa ya msanii huyu wa Injili, akichoma moto gari alilopewa kama zawadi na Nabii GoerDavie wa Arusha, baada ya tukio hilo madai ya watu mitandaoni walikuwa wanasema kwa kudai ameibiwa nyota yake na Nabii huyo.