Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gozbert gumzo, kisa kuchoma moto gari

Gozbert Pict

Muktasari:

  • Kwenye video inayosambaa sana mitandaoni, mwimbaji huyo amefichua kuwa, alipokea gari hilo Desemba 2021, lakini aliamua kuliteketeza akieleza kuwa halikuendana na imani yake.

NYOTA wa muziki wa nyimbo za Injili nchini, Goodluck Gozbert, amezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuchoma gari alilodai kupewa zawadi na nabii, akidai zawadi hiyo haikuwa sahihi kwake.

Kwenye video inayosambaa sana mitandaoni, mwimbaji huyo amefichua kuwa, alipokea gari hilo Desemba 2021, lakini aliamua kuliteketeza akieleza kuwa halikuendana na imani yake.

"Video hiyo inaonyesha gari nililopewa zawadi na nabii hapa Tanzania wakati wa ibada Desemba 2021. Nina mengi ya kusema, lakini kwa sasa nataka kufafanua kuwa chakula nilichokula wakati wa ibada hiyo na gari nililopokea kama zawadi havikumpendeza Mungu ninayemtumikia. Madhabahu hayo hayakuwa sahihi kwangu kuwa sehemu yake," alisema Gozbert na kuongeza;

"Nafahamu video hii itazua hisia tofauti kwa wanaonipenda na wasionipenda, na naheshimu maoni yote. Ikiwa Mungu atanipa neema ya kusema zaidi, nitasema. Kwa sasa, naachia hapa. Mungu awabariki nyote."


Uamuzi wa msanii huyo kuchoma gari hilo umeigawa jamii, wengine wakimsifu kwa uthubutu wake wa kusimama imara katika imani yake, huku wengine wakizua maswali kuhusu umuhimu wa kitendo hicho.

Goodluck Gozbert anafahamika kwa nyimbo maarufu kama Amen, Hauwezi Kushindana, Nimesamehe, Shukurani na nyinginezo.