Ferre Gola, Mbosso kupamba mashindano ya Miss East Africa

Ferre Gola, Mbosso kupamba mashindano ya Miss East Africa

Dar es Salaam. Mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kongo, Ferre Gola na Yusufu Mbwana 'Mbosso' kutoka Tanzania watapamba shindano la Miss East Africa.

Hayo yamesemwa leo Jumanne 14,2021 na mratibu wa mashindano hayo,Hellen Kazimoto, katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 24 ukumbi wa Mlimani City.

Kazimoto amesema mbali na warembo kupita jukwaani siku hiyo, kutakuwepo na burudani na kuwataja wasanii hao kuwa ndio watalipamba shindano hilo.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa kampuni ya Rena ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo, Jolly Mutesa, amesema washiriki kutoka nchi 14 zitashiriki na kuzitaja kuwa ni pamoja na Moritius, Sudani ya Kusini, Djbout, Elitrea, Shelisheli, Comoro, na Uganda.

Nchi nyingine ni Kenya, Uganda, Malawi, Somalia, Ethiopia, Burundi, Ruanda na wenyeji Tanzania.

Jolly amesema mshindi katika mashindano hayo atapata zawadi ya gari aina ya Nissan Xtrail  na mshahara wa mwezi mmoja wa dola 1500, wakati mshindi wa  pili ataondoka na na kitita cha  dola 5000 huku mshindi wa tatu atapata dola 2000.

Akizungumza kama mdhamini mkuu wa shindano hilo, kutoka kampuni ya Wasafi, Jamal April amesema katika mashindano hayo warembo wanaangaliwa katika mambo mbalimbali na sio uzuri tu wa sura na umbo bali kujiamini,  namna ya  kuweza kutangaza nchi zao na bara la Afrika kwa ujumla na kufanya programu mbalimbali za kusaidia jamii.