Fantasia kama Jennifer Hudson

Fantasia
LOS ANGELES, MAREKANI
MWANAMUZIKI Fantasia Barrino amesema anajipunguza ili awe mfano kwa familia yake na watu wengine wenye uzito mkubwa kwa kuwa si jambo jema kuukumbatia ‘unene’.
Fantasia ambaye hivi karibuni alijitokeza akiwa amepungua uzito muda mfupi baada ya kujifungua, amesema alifanya mazoezi na kuzingatia mlo bora ili kujipunguza.
“Mazoezi ni kama sala kwangu, lazima nifanye mara tatu kwa siku, kuzingatia chakula pia jambo ninalolipa kipaumbele, nataka kuwa mfano kwa familia yangu na jamii yote,” anasema Fantasia.
Mwaka juzi mwanamuziki na mwigizaji mshindi wa tuzo ya Oscar, Jennifer Husdon alijipunguza uzito kwa kiasi kikubwa naye akitoa sababu zinazofanana na za Fantasia.