Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ESHE BUHETI: Mimi na Shilole tumemalizana

Bukheti Pict
Bukheti Pict

Muktasari:

  • Mbali na hilo, staa huyu wa Bongo Movie, Eshe Buheti  anatamba na filamu nyingi na shughuli hizo ndizo zinazomuweka mjini, mapishi, filamu.

KUIGIZA ni kipaji, ila kupika sasa... Acha kabisa. Ukitaka kudhihirisha hilo, tembelea tu ukurasa wake wa Instagram. Utagundua ni mjasiriamali kweli.

Mbali na hilo, staa huyu wa Bongo Movie, Eshe Buheti  anatamba na filamu nyingi na shughuli hizo ndizo zinazomuweka mjini, mapishi, filamu.

Dakika 5 Na... ilipata nafasi ya kuzungumza na Eshe na kufunguka mambo mengi kuhusu maisha yake, ikiwamo bifu lake na Shilole na hadi kulimaliza, mume wake na mambo ya sanaa alikofikia sasa.


Mwanaspoti: Hongera kwa kumaliza ugomvi na Shilole, vipi kauli ya kutokukuzika bado unayo kwake?

Eshe Buheti: Asante. Hata Mungu anapenda watu waelewane muda wote, hivyo ile kauli ya nikifa asinizike bwana weee.. zile zilikuwa hasira tu, kama yeye alivyoniambia mimi sio Mtanzania. Kwa hiyo mambo tushayamaliza na hasira zimeisha. Kwa sasa hata kwenye msiba wangu aje na wosia asome sina tatizo naye.

BK01
BK01

Mwanaspoti: Ila baada ya kupatana kwenye msiba ulifanya ukiongea na vyombo vya habari ulisema pamoja na kupatanishwa ila huwezi kumsamehe Shilole. Hii ilikuwaje tena ikiwa mambo mlishayamaliza?

Eshe Buheti: We achana na haya mambo bana. Jua tu mambo yameisha, ndiyo maana sitaki tena kufanya 'interview' juu ya hayo mambo, unajua kuna vitu vingi vya kufanya eee!.


Mwanaspoti: Kuna changamoto yoyote unapata baada ya mume wako, Ahmed Wazir kutemwa na Singida Big Stars kwenye usajili wa msimu huu wa Ligi Kuu Bara?

Eshe Buheti: Changamoto zipo nyingi tu. Kwanza mimi nilikuwa sijui kama watu wanamfatilia sana, nimegundua baada ya kumposti na kupata 'comment' za baadhi ya watu za kejeli zikisema kwa sasa hana timu atauza chakula tu kwenye mgahawa, mara zingine zinasema ananenepa tu sababu sasa hivi hana timu.

Zipo nyingine zikiniuliza hachezi tena mpira? Lakini mie nasema tu, Mungu yupo pamoja nasi, hivyo Inshaalah atapata tu timu, kwani usajili bado unaendelea, si kuna dirisha dogo? Tuombe uzima na dua kwa sana tu, ila hizo 'comment' zao za kejeli na matusi nachukulia kama ni changamoto kwetu.

BK02
BK02

Mwanaspoti: Kuna madai umetoka kwenye ndoa ya kwanza na mume wako ambaye alikuwa mtu mzima na ukaamua kuolewa na kijana ambaye wewe ndiye tegemezi wa kila kitu.

Eshe Buheti: Hakuna kitu ambacho sikipendi kama hizi habari za kumjadili mume wangu, yaani naona wanamkosea sana heshima, niwaombe watu wamheshimu sana mume wangu. Ni mwanamume anayejiweza na kujali, kiufupi anatimiza majukumu yake kama mume, hivyo watu waache kumwongelea tofauti.


Mwanaspoti: Timu yako ni ipi? Au Singida Big Stars (Sasa Singida Black Stars?

Eshe Buheti: Weeee mimi ni Yanga, pamoja na mume wangu alikuwa Singida Big Stars na huwezi amini huwa nilikuwa napata wakati mgumu sana siku Yanga na Singida zikicheza maana huku nataka kushangilia timu yangu na huku nataka kumshangilia mume (kicheko).


Mwanaspoti: Ulikutana wapi na Ahmed?

Eshe Buheti: Nilikutana na mume wangu tangu akiwa anacheza Mbeya City, kabla hajahamia Singida Big Star. Nakumbuka ilikuwa Sinza sehemu moja wanachoraga tattoo na mwenye hiyo sehemu ni rafiki wa mume wangu. Hapo nilikuwa sijui, mimi nilienda kutengeneza vipini vyangu, rafiki wa mume wangu akaniposti, ndipo mume wangu akaanza kuchati na rafiki yake kuhusu mimi, mara nikaona amekuja nilipo na kuongea naye.

Lakini mimi nilipomaliza shughuli zangu nikaachana nao, hapo nikarudi zangu nyumbani, usiku nikaona ujumbe Instagram Ahmed amenitumia namba yake, hapo ndipo tukaanza kuwasiliana japo haikuwa rahisi siku hiyo hiyo kuwasiliana nilikaa muda kidogo ndipo nikaanza kumtafuta kwenye ile namba yake na hadi tukaja kuoana yalipita mambo mengi.

BK03
BK03

Mwanaspoti: Nani aligundua kipaji chako cha uigizaji?

Eshe Buheti: Mtu mwenye mchango mkubwa kwangu ni msanii  mkongwe, Issa Mussa ‘Cloud 112. Ndiye prodyuza wa kwanza kunichezesha na kunitambulisha kwenye uigizaji. Hapo ndipo wasanii wakongwe wengine walipoona kipaji changu na kuanza kunitumia. Nilishawahi kupata tuzo ya msanii bora wa kike kupitia Filamu ya ‘Mimi na Mungu Wangu’. Tuzo hizo  zilizotolewa na ZIFF katika Tamasha la Kimataifa la Filamu la Nchi za Jahazi ‘ZIFF’ lililofanyika mjini Unguja, Zanzibar mwaka 2015.

Nashukuru sana kupata tuzo ile. Kwa ushindi ule nilipata mkataba Kenya ambako kuna tamthilia nilishiriki inaitwa Kashfa, imechezwa zaidi na Wakenya, lakini kwa upande wa Tanzania, nilikuwa mimi na Yusuph Mlela.

Hao jamaa wa hiyo tamthilia walinikubali baada ya kuniona ZIFF nikichukua tuzo na kazi nilizofanya.


Mwanaspoti: Vipi kwa sasa kuhusu filamu?

Eshe Buheti: Naendelea kuigiza, pia huwa naingiza sauti katika tamthilia tofauti za hapa nyumbani zinazoruka kwa Lugha ya Kiswahili.


Mwanaspoti: Una watoto?

Eshe Buheti: Ndiyo nina watoto wawili ambao nimewapata kabla ya ndoa yangu hii ya pili, nimezaa na mume wangu wa kwanza.