DJ Sinyorita abeba Afrima

Monday November 22 2021
sinyo pic
By Nasra Abdallah

Mwanaisha Said maarufu kwa jina la DJ Sinyorita, ameipaisha Tanzania baada ya kushinda tuzo ya Afrima.

Tuzo hizo zimetolewa usiku wa jana Jumapili Desemba 2, 2021 nchini Nigeria.

Katika tuzo hizo, Sinyorita ameshinda kipengele cha Dj bora Afrika akiwabwaga wengine kumi aliokuwa akishindanishwa nao.

Ma Dj hao  na nchi wanazotoka kwenye mabano DJ Moh Green (Algeria), Black Coffee (South Africa), DJ Cuppy (Nigeria), DJ Impossible (Angola) ,DJ Kaywise (Nigeria) na DJ Mix Premier (Ivory Coast)

Wengine ni DJ Sly (Ghana), DJ Spinall (Nigeria) na Major League DJz (South Africa).

Hata hivyo watanzania wengine waliotajwa kwenye tuzo hizo walitoka patupu, akiwemo msanii nyota wa Bongofleva, Diamond Platnumz aliyekuwa akishindanishwa kwenye kipengele cha msanii bora wa mwaka na  msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.
 
Wengine waliokuwepo ni Rosa Ree, aliyekuwa akiwania vipengele vitatu ikiwemo  cha Msanii bora wa Hiphop, msanii wa muziki wa Raggae Dancehall (That Girl) na msanii bora wa kike Afrika Mashariki.

Advertisement

Pia wasanii wengine walikuwepo ni  Zuchu, Nandy,  Alikiba, Harmonize, Darasa, Rayvanny na Director Kenny.

Advertisement