Diamond Platnumz aandika historia shoo ya England

Muktasari:
- Hii ni mara ya kwanza kwa msanii kutoka Afrika Mashariki kufanikisha kujaza mashabiki wengi katika ukumbi huo wa kifahari, ambao wamewahi kupanda wasanii wakubwa duniani kama Adele, Beyonce na Ed Sheeran.
MSANII nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz', ameandika historia usiku wa kuamkia Ijumaa kwa kutumbuiza katika ukumbi maarufu duniani wa Royal Albert Hall, London, Uingereza.
Hii ni mara ya kwanza kwa msanii kutoka Afrika Mashariki kufanikisha kujaza mashabiki wengi katika ukumbi huo wa kifahari, ambao wamewahi kupanda wasanii wakubwa duniani kama Adele, Beyonce na Ed Sheeran.

Shoo hiyo ilikuwa sehemu ya ziara ya kimataifa ya Diamond World Tour 2025, ikiingiza maelfu ya mashabiki kutoka sehemu mbalimbali za Uingereza na bara la Ulaya.
Kwa mujibu wa uongozi wa Royal Albert Hall, tiketi zote ziliuzwa mapema hali iliyosababisha uongozi wa ukumbi huo kumpa Diamond cheti maalum cha "Sold-Out Show" kama ishara ya mafanikio ya kipekee.
Diamond alifika jukwaani akiwa amefuatana na wasanii kadhaa wa kimataifa akiwamo Juma Jux kutoka Tanzania, Mr Flavour na Tiwa Savage kutoka Nigeria na Patoranking.
Wakali hao walitumbuiza kwa zaidi ya saa mbili, wakitoa burudani iliyogusa nyoyo za mashabiki kwa mchanganyiko wa muziki wa Bongo Fleva, Afrobeats, R&B na midundo ya kiafrika ya asili.
Diamond aliimba nyimbo zake maarufu kama Jeje, Yatapita, Mtasubiri na Number One akionyesha uwezo wake wa kuimba moja kwa moja (live performance), muonekano wa kisasa na sauti safi vikizidi kuthibitisha nafasi yake kama mfalme wa muziki Afrika Mashariki.

Kitendo cha Diamond kuujaza ukumbi huo yatafungua milango kwa wasanii wengine wa Afrika Mashariki kufanikisha ndoto zao kimataifa.
Miongoni mwa watu waliompongeza msanii huyo ni Zuchu anayemsimamiwa na lebo ya Wasafi ambaye aliandika: "MUMEWANGUUUUUUU SIIIMBAAAAAAAAA, Yooooooh This Is #SWAHILINATION Its About time EAST AFRICA GETS ITS OWN SHINE, EAST AFRICA’s FINEST THE HERO YOH @diamondplatnumz AM SHAKING SIWEZI HATA ANDIKA BUT YOH. AISEEE YOU ARE GOD GIVEN UMEBARIKIWA SANA. KEEP SOARING LION KEEP PAVING THE WAY FOR US. HAIJAWAHI KUTOKEA TODAY BONGOFLAVOR IS WINNING. I AM SO HAPPY."

Barnaba aliandika "BIG | MAN ON THIS ONE @diamondplatnumz. LION. MASTER BINAFSI I AM SO PROUD OF YOU MY BROTHER KEEP OPEN THE DOOR. TANZANIA STAND UP. NASIBU MTU BINGWA KABISA KILA NIKIANGALIA HIZI LIST ZA ARTIST KUTOKA MATAIFA MBALI MBALI WAKIKARIBISHWA NA MZEE | HAPA NDO UTAGUNDUA HOW NASIBU IS BIG 🙌🙌."
Msanii Madee alisifu: "Kwangu mimi hii ndio habari kubwa ya leo... Labda kwasababu ipo kwenye eneo la kazi yangu... vingi nimevutiwa navyo kwenye hii show kubwa ya @diamondplatnumz kama vile surprise ya @tiwasavage @patorankingfire na wengine wengi... lakini lililonivutia zaidi ni kwenda na @juma_jux hawa wenzetu Wanaijeria huu ndio ulikuwa mtindo wao wa kufikishana juu mpaka wakapatikana wengi kimataifa. Show ya Davido lakini tunaweza kumuona TEKNO...
"Show ya WIZKID lakini tunaweza kumuona OMAH LAY ... @diamondplatnumz anaonyesha namna gani unaweza ukaenda peke yako na ukafanikiwa... lakini pia unaweza kwenda na wenzako mkafanikiwa zaidi... congratulation Naseeb show nzuri.. nimependa hii movement yako... Next mchukue @dogo.paten or @dullamakabila ili wazungu wakautambue rasmi mziki wa Singeli... Oya wanahabari hii ndio habari kubwa ya leo.. mambo ya kina Mnguto tushamalizana nayo. Twendeni na hii..."