Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond, Erick Omondi kimewaka

Omondi Pict

Muktasari:

  • Ili kujulikana kwa ukubwa Tanzania, Eric Omondi aliweka ukaribu na Diamond ikiwamo kutengeneza video za vichekesho akiigiza kazi za bosi huyo wa WCB na alionekana kuwa na ukaribu na Mondi lakini sasa mambo yamechukua sura mpya.

STAA wa Bongofleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz amemjibu msanii wa vichekesho nchini Kenya, Erick Omondi kufuatia kauli yake kuwa wasanii wanapendelewa wakifanya shoo nchini humo.

Ili kujulikana kwa ukubwa Tanzania, Eric Omondi aliweka ukaribu na Diamond ikiwamo kutengeneza video za vichekesho akiigiza kazi za bosi huyo wa WCB na alionekana kuwa na ukaribu na Mondi lakini sasa mambo yamechukua sura mpya.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Omondi aliandika: "Nimeshuhudia mara nyingi wasanii wa Kenya wakiomba mlangoni kwa maaskari wa usalama ili kuruhusu timu yao (mameneja na madansa) kuingia ukumbini huku ndugu zetu wa kimataifa wakifika kwa misafara ya magari hadi 15.

"Kuna mengi yanaendelea nchini Kenya leo lakini jambo moja nina hakika, mengi yanaendelea kubadilika tutavuna, wakati wetu umekaribia."

Baada ya ujumbe huo Diamond akaamua kumjibu kupitia mtandao huo huo akiandika hivi: "Kaka yangu Eric, mafanikio hayaji kwa kuwawekea chuki wengine, bali yanakuja kwa kuongeza juhudi kisha Mungu naye atakubariki. Wewe ni moja ya mfano mzuri kwenye hili, ulishakuja zaidi ya mara 10 Tanzania kufanya matamasha na siku zote ulipokewa kwa upendo, hukuwahi kusikia Standup Comedians wakikuletea chuki ama kusikia wakisema "wanaonewa' wala campaign za "We want 75% kwa makomedi wa Tanzania".

"Walijitathmini wakaona nini wafanye ili nao kufanikiwa, wakaweka bidii, zikaanzishwa ChekaTu, Watu Baki na majukwaa mbalimbali ya wachekeshaji wa standup ambazo zikazalisha, na leo hii nao wananufaika na kazi zao. Juzi tu alikuja Biensol Tanzania na watu wamempokea kwa upendo na kufanya kazi na wasanii mbalimbali. Afrika Mashariki ni nchi zinazoishi kwa upendo na ushirikiano, jitahidi kuhamasisha upendo na ushirikiano na kuweka bidii, instead ya kuwafunza wasanii watuwekee chuki maana sio njia ya kufanikiwa," alimaliza hivyo.

Mvutano ulitokea jijini Nairobi baada ya Diamond kushindwa kutumbuiza kwenye tamasha la Furaha City Festival lililofanyika nchini humo kufuatia tafrani iliyoibuka kati yake na msanii wa Kenya, Willy Paul.

Vyombo vya habari jijini Nairobi viliripoti kuwa hekaheka zilianza pale ambapo Willy Paul alizuiwa kupanda jukwaani licha ya ratiba kuonyesha kwamba alitakiwa kupanda jukwaani kabla ya Diamond Platnumz.

Baada ya kutokea fujo hizo, Diamond ilibidi aahirishe kufanya onyesho lake uwanjani baada ya meneja wake Sallam SK kupiga simu na kumtaka asitumbuize.

Video zilizosambaa mitandaoni zilimuonyesha Willy Paul akivutana na walinzi pamoja na uongozi wa steji akipambana kuzuia Diamond Platnumz asipande kutumbuiza kwa kuwa haukuwa muda wake.

Wakenya walionekana kutopendezwa na uamuzi huo wa Diamond kupanda kabla ya Willy Paul na walianza kurusha maneno wakiimba jina la (Pozee) wakati mshereheshaji akitaka kumpandisha Diamond Platnumz.

Baada ya mvutano ilibidi meneja wa steji ampandishe Willy Paul kama ilivyokuwa imepangwa, lakini baada ya onyesho lake alijikuta hawezi kuondoka uwanjani pale kwani magari yake yalikuwa yamezuiwa kwa maelekezo maalum.

Willy Paul alionekana hata kumgeuka Rayvanny ambaye alishirikiana naye katika wimbo uliotamba wa Mmmh!, ambapo DJ alipoanzisha beat la wimbo huo wakati Willy Paul akiwa stejini, staa huyo wa Kenya alisema "We Dj, Dj, Dj... toa hiyo takataka, tupatie the next song."

Wakati wa Willy Paul akitaka kupanda stejini, ililalamikia kupigwa na baunsa wa Diamond, huku msanii na mtangazaji wa Wasafi Radio, Baba Levo akisema atamuongeza bonasi baunsa huyo na wengine kwa kazi nzuri akidai mtu hawezi kuvuruga shoo ya msanii mkubwa halafu aachwe hivi hivi.

Baba Levo katika video aliyojirekodi, alisema Diamond kabla ya kusaini mkataba huwa anaandikishiana muda wa kupanda stejini na muda wa kushuka na moja ya masharti ni kwamba lazima ukumbi uwe umejaa ndio atapanda hivyo mwandaaji ni lazima afanye promosheni ya kutosha ya kujaza shoo yake. "Kwa sababu tumeshaenda kwenye baadhi ya shoo ambako hamna mashabiki halafu ikatuletea shida, hivyo ni lazima ukumbi uwe umejaa ndio Diamond atapanda stejini."

"Diamond ni lazima apangishiwe hoteli ya kuanzia nyota tano, yeye na timu yake nzima, hata kama watakuwa 30, sio uwaweke madansa wake au mabaunsa kwenye gesti za vichochoroni," alisema Baba Levo, huku akijitambulisha kama chawa wa Diamond na CEO wa 7 Media.