Filamu ya The Royal Tour yachochea ongezeko la watalii nchini

Muktasari:
- Filamu hiyo imesaidia Tanzania kufahamika zaidi kimataifa, kwani ilionyesha madhari mazuri na rasilimali nyingi ambazo Tanzania imejaliwa.
Ikiwa imepita miaka mitatu tangu, tangu Rais Samia Suluhu Hassan azindue filamu ya ‘The Royal Tour’ filamu hiyo imeendelea kuchagiza ongezeko la watalii nchini
Filamu hiyo imesaidia Tanzania kufahamika zaidi kimataifa, kwani ilionyesha madhari mazuri na rasilimali nyingi ambazo Tanzania imejaliwa.
Hiyo amesaidia kukuza sekta ya utalii, ambapo idadi ya watalii kutoka nje ya nchi imeongezeka kutoka 922,692 mwaka 2021 hadi watalii 2,141,895 mwaka 2024 ambayo ni sawa na asilimia 132.1.
Watalii wa ndani nao wameongezeka kutoka watalii 788,933 mwaka 2021 hadi kufikia watalii 3,218,352 mwaka 2024 ambayo ni sawa na 307.9%.
Kupitia sekta ya utalii nchini, Tanzania imevuna Sh10 trilioni. Ambazo zimesaidia kukuza sekta ya ajira kwani idadi ya wakala wa utalii imeongezeka kutoka mawakala 2,885 (2020) hadi mawakala 3,735(2025), huku idadi ya waongoza watalii ikiongezeka kutoka 5,076 hadi 7,862 sawa na ongezeko la 55%.
Hii ni wazi kuwa miaka minne ya Rais Samia sekta ya utalii imepiga hatua, huku Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) lilitwaa jumla ya tuzo saba za (World Travel Awards 2025) kwa Ukanda wa Afrika na Bahari ya Hindi, Tanzania ikishinda jumla ya tuzo 20 tukio lililoweka Tanzania kwenye ramani ya utalii duniani kwa mara nyingine.