Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond ashindwa kujizuia, awachana wanamponda

Muktasari:

  • Mond aliyasema hayo usiku wa kuamkia jana alipokuwa jukwaani  huko, Ruangwa Lindi katika shoo ya Wasafi Festival 2024, baada ya baadhi ya watu kumkejeli kwa kauli aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa tamasha la Wasafi Festival 2024, ndoto aliyonayo ni kuwa utajiri namba moja duniani na kusema inawezekana, kwani kwenye maisha hakuna kukatishwa tamaa.

SUPASTAA wa muziki wa Bongo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ameshindwa kujizuia na kuamua kuwajibu watu waliomkejeli na kumbeza kuhusu kauli aliyotoa ya ana ndoto ya kuwa tajiri namba moja duniani, hajali maneno ya watu na hawezi kukata tamaa hadi aifanikishe.

Mond aliyasema hayo usiku wa kuamkia jana alipokuwa jukwaani  huko, Ruangwa Lindi katika shoo ya Wasafi Festival 2024, baada ya baadhi ya watu kumkejeli kwa kauli aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa tamasha la Wasafi Festival 2024, ndoto aliyonayo ni kuwa utajiri namba moja duniani na kusema inawezekana, kwani kwenye maisha hakuna kukatishwa tamaa.

Alisema mwaka 2018  aliwaambia watu,  moja ya vitu anavyotakiwa kuvifanya ni kutaka kununua gari la kifahari aina ya Rolls Royce, watu waliongea na kumponda wakimwambia hataweza, lakini alinunua mwaka huo huo tena likiwa ziro kilomita.

“Mimi nawaambia kila kitu kwa uwezo wa Mungu hakishindikani na siwezi kukatishwa tamaa na watu,” alisema.

Diamond alisema, Rolls Royce hadi inafika Tanzania ilitumia Dola 974,000 ambazo ni zaidi ya Sh 2 bilioni, hivyo miongoni mwa vitu ambavyo Watanzania wanatakiwa kujivunia ni kuwa naye maana anapamba sana yote kwa sababu ya sapoti zao.

Alisema watu wafahamu pale nyumbani kwake kuna gari imepakiwa ina thamani ya Sh2.7 Bilioni anayotembelea tu, angeweza kusikiliza maneno ya watu na kejeli asingeweza kununua, hivyo  watu wasikubali kuambiwa kitu ulichopanga hakiwezekani.