Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

D Voice ajibebisha kwa Yammy

Muktasari:

  • D Voice amefunguka hilo juzi kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam baada ya kushuka kufanya kujwaani kufanya shoo ambayo Yammy naye alitumbuiza n alipoulizwa juu ya kufanya kolabo na mwanadada huyo naye alisema yu tayari, lakini anampenda pia kimapenzi.

NYOTA wa miondoko ya Bongo Fleva na Singeli nchini, D Voice kutoka lebo ya WCB Wasafi, amekiri hadharani kwamba anamzimia msanii mwenzake chipukizi, Yammy na anatamani awe mpenziwe.

D Voice amefunguka hilo juzi kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam baada ya kushuka kufanya kujwaani kufanya shoo ambayo Yammy naye alitumbuiza n alipoulizwa juu ya kufanya kolabo na mwanadada huyo naye alisema yu tayari, lakini anampenda pia kimapenzi.

“Nashukuru leo tumekutana jukwaa moja na mwimbaji  ninayemkubali sana katika kuimba na sio tu kuimba, hata awe mpenzi wangu, siku nyingi nampenda Yammy, natamani itokee awe mpemzi wangu,” alisema D Voice

Kwa upande wa Yammy, anayetokeaLebo ya The African Princess ya Nandy, alipoulizwa juu ya msimamo huo wa D Voice kuwa anapenda ajibebishe kwake, naye aliishia kuijibu neno moja tu. ‘Nashukuru’.

Hata hivyo, D Voice hivi karibuni ameingia katika skendo ya kujihusisha kimapenzi na mwanadada Lulu Diva japo kila mmoja amekuwa akikwepa kuweka ukweli bayana na kuwaacha mashabiki njia panda.

Mwimbaji huyo ni msanii wa saba kutambulishwa na WCB Wasafi baada ya Harmonize (2015) Rayvanny (2016), Rich Mavoco (2016), Lava Lava (2017), Mbosso (2018) na Zuchu 2020.  Rich Mavoko, Harmonize na Rayvanny wameshajitoa kwenye lebo hiyo na kujitegemea.